Unknown Unknown Author
Title: AZAM WAFANIKIWA KUMSAJILI MCHEZAJI HATARI WA YANGA
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Didier Kavumbagu akitia gole gumba kuichezea Azam FC kwa miaka miwili. Mshambuliaji wa zamani wa klabu ya Yanga Didier Kavumbagu ametia...
KAVUMBAGU
Didier Kavumbagu akitia gole gumba kuichezea Azam FC kwa miaka miwili.

Mshambuliaji wa zamani wa klabu ya Yanga Didier Kavumbagu ametia dole gumba katika mkataba na Azam FC ili aitumikie kwa mwaka mmoja baada ya kumaliza mkataba wake na Yanga aliyo ichezea kwa misimu miwili.

Kavumbagu ambaye ni Nahodha wa Burundi alitua Yanga mwaka 2013 akitokea Atletico ya nchini kwao na ameweza kuifungia klabu yake ya zamani Yanga mabao 31 katika michezo 63 aliyocheza.
“Mimi sasa ni mchezaji wa Azam, nafurahi kujiunga na klabu hii kubwa. Kawaida yangu huwa nashabikia klabu nayochezea, sasa mimi ni mshabiki namba moja wa Azam,”amesema Kavumbagu

Mchezaji huyo alimaliza mkataba wake na Yanga lakini viongozi wa klabu hiyo hawakutaka kumuongezea mkataba wala kukaa na kuongea naye toka ligi imalizike, kwa kuwa maisha yake ni mpira Kavumbagu leo ameamua kuhama makazi na kukimbilia Chamazi kwa wana lambalamba.

About Author

Advertisement

Post a Comment Blogger

Toa Maoni Yako Kuhusu habari Hii

Note: Only a member of this blog may post a comment.

 
Top