MIRALLAS AMBANIA ADINAN JANUZAJ KOMBE LA DUNIA

ADINAN JANUZAJ
Adinan Januzaj
Na. Paul Manjale
Winga wa klabu ya Everton na timu ya taifa ya Ubelgiji Kevin Mirallas amemtaka amemtaka kocha wa timu hiyo Marc Wilmots kumtomjumuisha kikosini kinda wa Manchester United Adinan Januzaj (19).Mirallas ambaye kwa sasa yuko nje ya uwanja akiuguza majeraha ya misuli amesema haitakuwa ni jambo la busara kwa kinda huyo kuwemo katika kikosi kitakachoiwakilisha Ubelgiji katika fainali zijazo za kombe la dunia nchini Brazil.

Mirallas anasema "Nimefurahi kusikia Januzaj amechagua kuchezea Ubelgiji na kuzitosa Albania,Cosovo na Serbia lakini sidhani kama huu ni muda muafaka kwa yeye kuwemo kikosini.Hajacheza mechi za kutosha miezi ya karibuni pia si mtu anayejua mengi yanayoendelea hapa. Pia nafasi anayocheza ina wachezaji wengi na wazuri hivyo itakuwa ni ngumu kwake kupata nafasi. 


Namshauri asubiri mashindano yajayo ya Ulaya mwaka 2016 huku akipambana kuhakikisha anakuwa na namba ya kudumu katika nafasi anayocheza katika kikosi cha United"

Post a Comment

Hii ni Blog kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Nchi yetu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...

Previous Post Next Post