Unknown Unknown Author
Title: LADY JAY DEE “MIMI NA GADNER TUNAISHI KAMA KAKA NA DADA”, SOMA UNDANI WA HABARI HII
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Super woman katika Afro-Pop, Judith Wambura a.k.a Lady Jaydeee au Jide katika pozi na mume wake Gardner Habash ‘Kapteini’ . Kumbe! Super w...

clip_image001Super woman katika Afro-Pop, Judith Wambura a.k.a Lady Jaydeee au Jide katika pozi na mume wake Gardner Habash ‘Kapteini’ .

Kumbe! Super woman katika Afro-Pop, Judith Wambura a.k.a Lady Jaydeee au Jide amefunguka kuwa yeye na mumewe, Gardner Habash ‘Kapteini’ kwa sasa wanaishi kama kaka na dada hivyo kuibua swali kivipi?

clip_image001[7]Akizungumza na Ijumaa Wikienda katika mahojiano maalum yaliyofanyika kwenye mgahawa wa staa huyo wa Nyumbani Lounge uliopo Ada Estate, Kinondoni jijini Dar mwishoni mwa wiki iliyopita, Jide alisema kuwa yeye na Gardner wamefikia hatua ya kuishi katika staili hiyo kutokana na mapenzi yao yaliyopitiliza.

“Gardner ananipenda sana na mimi pia vilevile nampenda sana mume wangu. Mapenzi yetu yamepitiliza hadi tunajiona kama vile tumezaliwa tumbo moja na ndiyo maana nawaambia kuwa mimi na yeye tunaishi kama kaka na dada,” alifunguka Jide.

clip_image001Akiendelea kuzungumza kwa kujiamini, Jide alisema kuwa hadi simu ya mkononi wanatumia moja kwa ajili ya mawasiliano.
“Mimi hapa sina simu, anayo mume wangu lakini wakati mwingine nakuwa nayo mimi ila muda mwingi anakuwa nayo Gardner,” alimalizia Jide.

>>GPL

About Author

Advertisement

Post a Comment Blogger

Toa Maoni Yako Kuhusu habari Hii

Note: Only a member of this blog may post a comment.

 
Top