Unknown Unknown Author
Title: WIZARA YA AFYA KUREJESHA KOZI YA MAAFISA AFYA NGAZI YA CHETI
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Na Elvan J. Limwagu , Morogoro Naibu Katibu Mkuu (Afya) Wizara ya Tawala za Mikoa na Serikali za Mikoa (TAMISEMI) Dkt. Deo Mtasiwa amesema ...

LIMWAGUNa Elvan J. Limwagu, Morogoro

Naibu Katibu Mkuu (Afya) Wizara ya Tawala za Mikoa na Serikali za Mikoa (TAMISEMI) Dkt. Deo Mtasiwa amesema kuwa Kada ya Maafisa Afya ya Mazingira ngazi ya Cheti iko mbioni kurejeshwa wakati wowote kuanzia sasa ili kuendelea kuzalisha Mabwana Afya Wasaidizi kwa ngazi ya Kata na Vijiji.

Akiongea na wakati wa kufunga kikao cha kazi cha Maafisa Afya wa ngazi za Mikoa na Halmashauri mbalimbali nchini waliokutana kwa muda wa siku 3 kuanzia tarehe 29 Januari 2014 katika ukumbi wa BZ uliopo Mjini Morogoro.

Akifafanua zaidi Dkt. Deo Mtasiwa alisema kuwa maamuzi yaliyofanywa na Wizara ya AFya ya kuondoa kozi hiyo na kuvifunga vyuo vyake yalifanywa kimakosa kwani ndipo wanapozalishwa wataalamu wa ugani na kwamba walikuwa wanasaidia kutekeleza kazi mbalimbali za usafi wa mazingira na kinga ya magonjwa ya kuambukiza na yasiyo ya kuambukiza kuanzia ngazi ya chini na hatimaye ngazi za wilaya, mikoa na wizara kupata taarifa za haraka.LIMWAGU 2Kikao hiki pia kilitumika kutathmini shughuli za Kampeni ya Usafi wa Mazingira inayoendeshwa hivi sasa nchini kuanzia mwaka 2012 kwa kuhusisha Halmashauri zote nchini sanjari na kufanya mapitio ya bajeti ya kampeni kwa mwaka ujao wa fedha.

Kikao hicho cha kitaalamu kilichofunguliwa na Ndugu Charles Palangyo ambaye ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii ulitoka na maazimio yafuatayo:

1. Sekretariet za Mikoa na Halmashauri zote zisimamie vema fedha zinazotolewa kwa ajili ya kampeni ya usafi wa mazingira.

2. Sekretariet za Mikoa na Halmashauri za Wilaya wafanye vikao vya kuhakiki taarifa za robo siku 5 kabla ya kuzituma Wizarani.

3. Watu wanaokusanya takwimu za usafi wa mazingira wapewe motisha ili wawe na morari ya kuendelea na kazi hiyo ambayo ni ngumu.

4. Sekretariet za Mikoa na Halmashauri ziwe na ushirikiano wa karibu kuweza kutekeleza shughuli zao kwa ufanisi.

5. Sekretariet za Mikoa na Halmashauri waweke mipango ya kuajiri watumishi wa fani ya afya ya mazingira.

6. Sekretariet za Mikoa na Halmashauri zote wawajengee uwezo watumishi waweze kukusanya takwimu za usafi wa mazingira.

7. Utekelezaji wa Kampeni ya usafi wa mazingira kila Jumamosi ya kwanza ya mwezi iendelee nchini kote kutekeleza agizo la Waziri mkuu

Kikao hicho kimehitimishwa rasmi leo kwa mkutano wa uchaguzi wa viongozi wa juu wa chama cha Maafisa Afya ya Mazingira nchini.

About Author

Advertisement

Post a Comment Blogger

Toa Maoni Yako Kuhusu habari Hii

Note: Only a member of this blog may post a comment.

 
Top