WATU sita, wakiwemo watoto wa familia tafauti,wakazi wa wilaya za
Ruangwa na Kilwa,mkoani Lindi,wamekufa katika matuko tafauti likiwemo la kula nyama ya Kasa.
Habari kutoka wilayani Kilwa na kuthibitishwa na watendaji wa kata
husika na Jeshi la Polisi mkoani hapa,zinaeleza kuwa vifo hivyo
vimetokea kata za Nanjirinji,Kilanjelanje na Lihimalyao,februari 10 na
11 mwaka huu.
Marehemu hao ni, Hassani makumba (25) mkazi wa kijiji cha Namitema, wilaya ya Ruangwa, aliyefia kata ya Nanjirinji, Faki Issa (5),Mussa Ramadhani (7), Idrisa Abdallah (6), Yusufu Hafidhi (1) na Salum Mzee (miezi 7) wakazi wa kata ya Lihimalyao, wilayani Kilwa.
Wakizungumza kwa njia ya simu na mwandishi wa mtandao huu, Mtendaji wa kata ya Nanjirinji, Aisha Namalungo ameeleza kuwa Hassani Makumba mwenyeji wa wilaya ya Raungwa amekufa kwa kukatwa kwa mapanga na watu wasiojulikana na mwili wake kugundulika siku ya pili yake ya februari 11/2014 asubuhi, ukiwa na majeraha mbalimbali.
Afisa mtendaji wa kata ya Lihimalyao,Hassani Mwalimu amesema watoto watano wa familia tafauti wamekufa kwa madai ya kula nyama aina ya kasa februari 10 mwaka huu.
Mwalimu alisema siku hiyo watoto wakiwa na wazazi wao walikula nyama aina ya Kasa aliokuwa amevuliwa kutoka katika Bahari ya Hindi iliyopo wilayani Kilwa.
"Hii nyama ya kasa imeliwa na wote wakiwemo watoto na wazazi wao, lakini cha kushangaza hao ndio wamepoteza maisha wakiwaacha wazee wao wakiendelea kupeta"Alisema mwalimu.
Pia, akaeleza kuwa mara baada ya kuona watoto hao wakipoteza mwelekeo, waliwakimbiza kwenye Zahanati kwa ajili ya kupatiwa huduma, lakini haikuweza kusaidia kitu kwani walipoteza maisha muda mfupi walipokuwa wakikimbizwa kupata huduma za matibabu.
Kaimu kamanda wa Polisi mkoani Lindi,SSP,Joseph Mfungomara, amekiri kwa Ofisi yake kupokea kwa taarifa ya vifo hivyo na kueleza Jeshi hilo linaendelea na uchunguzi wake.
Post a Comment Blogger Facebook
Toa Maoni Yako Kuhusu habari Hii
Note: Only a member of this blog may post a comment.