Naibu Mkurugenzi wa mradi wa champion akitoa mada kwa wanahabari wa mkoa wa Lindi katika warsha inayoendelea.Picha ya pamoja kati ya Naibu Mkurugenzi wa Mradi wa Champion na wana habari wa mkoa wa Lindi waliohudhuria warsha kuhusiana na sheria na Sera za ukatili wa kijinsiaBaadhi ya wanahabari wa Lindi wakiwa katika warsha ya ukatili wa kijinsia inayotolewa na mradi wa Champion
Na Abdulaziz Video,Mnazi Mmoja ,Lindi
Sekta ya Habari Imetakiwa kutoa elimu zaidi ya ukatili wa Kijinsia ili
kujenga Taifa lenye amani kwa wananchi Bila kujali Jinsia, Dini na
kabila Wito huo umetolewa na Dr Monica Mhoja, Naibu Mkurugenzi wa mradi wa Champion unaofadhiliwa na Usaid alipokuwa akitoa mada katika warsha ya wanahabari wa Mkoa wa Lindi inayoendelea katika Ukumbi wa Sakina Mnazi mmoja Manispaa ya Lindi
Dr Mhoja amebainisha kuwa sekta ya habari ina wajinu mkubwa kwa
kushirikiana na serikali na mashirika yanayotoa elimu juu ya
Unyanyasaji kijinsia Nchini ili kuwapa mwanga jamii kuweza kuchukia
vitendo hivyo ambavyo ni kinyume na haki za Binadamu.
“Wanahabari ni jukumu lenu kutoa hii kwa kuwa mnayo nafasi na fursa kubwa ya kuelimisha kwa kuwa vitendo hivyo vinaongezeka kila siku ikiwemo kupigwa, Ukeketaji na ndoa za utotoni ili kuondoa ubaguzi na ukatili huo na hivyo kupitia warsha hii matarajio ya Shirika la Champion ni kuondoa hali hizo kwa kupitia vyombo vya Habari ndio maana tumewakusanya kuwapa elimu”, Alimalizia Dr Mhoja
Lengo la warsha hiyo ni kuwajengea Uwezo na Uelewa wa sheria na sera za Nchi zinazohusisha masuala ya ukatili wa kijinsia.
Warsha hiyo pia Inaendeshwa na Ofisa mradi mwandamizi wa kutoka
kitengo cha mawasiliano mradi wa Champion, Bw Muganizi Mutta na tayari mafunzo hayo yametolewa kwa Wanahabari wa mkoa wa Mtwara
Post a Comment Blogger Facebook
Toa Maoni Yako Kuhusu habari Hii
Note: Only a member of this blog may post a comment.