BREAKING NEWS:NDEGE YA ETHIOPIAN AIRLINES YATEKWA,ANGALIA VIDEO NA PICHA HAPA

clip_image002Ndege iliyokuwa imetekwa

Rubani msaidizi wa ndege ya abiria ya shirika la ndege la Ethiopia ndiye aliyeiteka nyara.

Maafisa mini Geneva wanasema kuwa naibu huyo wa rubani alichukua usukani wa ndege hiyo rubani wake alipokwenda msalani kwa haja.

Tukio hilo inaripotiwa kutokea ndege hiyo aina ya Boeing 767-300 ilipokuwa ikipaa katika anga ya Sudan.

Rubani huyo msaidizi alibadili mkondo wa ndege hiyo iliyokuwa ikielekea Rome Italia ,na kuipaa hadi Uswisi alipoitua katika uwanja wa ndege wa Geneva.clip_image001Katika taarifa kwa vyombo vya habari shirika hilo linasema kuwa abiria wote 200 wako salama .

Ripoti ya idara inayosimamia usafiri wa ndege ya Uswisi inasema kuwa rubani huyo msaidizi aliomba uraiya kabla ya kutua ndege hiyo na akajisalimisha kwa maafisa wa usalama waliokuwa wameizingira ndege hiyo.

Polisi walimtia mbaroni mara moja .

Chanzo BBC Swahili

Post a Comment

Hii ni Blog kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Nchi yetu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...

Previous Post Next Post