KUTOKA MAHAKAMANI:: LULU AKANA KUMUUA KANUMBA, AKUBALI KUWA ALIKUWA NA MAHUSIANO YA KIMAPENZI

MSANII wa Filamu nchini, Elizabeth Michael'Lulu' ambaye anakabiliwa na kesi ya kumuua bila kukusudia msanii mwenzake, Steven Kanumba, amekiri kuwa alikuwa na uhusiano wa kimapenzi na msanii huyo na kwamba walikuwa na ugomvi.luluLulu alikiri hayo leo wakati akisomewa mashitaka yake mbele ya Jaji Rose Temba wa Mahakama Kuu, Kanda ya Dar es salaam ambapo lulu  baada ya kusomewa mashitaka amekana kumuua.

Mbali na kukiri kuwa na uhusiano, pia lulu akikiri kuwa baada ya tukio alitoka nje ya chumba walichokuwepo na kwenda kumwambia mdogo wake Marehemu Kanumba, Setti Bosco kuwa marehemu amedondoka.

Akisoma hati ya mashitaka Wakili Mwandamizi wa Serikali, Monica Mbogo, alidai kuwa Aprili 7, mwaka 2012, Sinza Vatikani, Mkoa wa Dar es salaam, mshitakiwa alimuua bila kukusudia msanii Kanumba.

Wakili Kombo, alidai kuwa pamoja na mambo mengine, marehemu Kanumba baada ya kufa, mwili wake ulipelekwa hospitali ya Taifa Muhimbili ambapo majibu yanaonyesha kwamba kifo chake kimesababishwa na uvimbe ndani ya ubongo.

Upande wa serikali una mashahidi watano pamoja na vielelezo wakati upande wa utetezi unatarajia kuwa na mashahidi watano na vielelezo.

CREDIT : PRO24

Post a Comment

Hii ni Blog kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Nchi yetu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...

Previous Post Next Post