MSANII KUTOKA KENYA NYOTA NDOGO AMPASUKIA MUSTAFA KWA VISANGA VYAKE NA HUDDAH, SOMA HAPA

Drama ya uhusiano kati ya Huddah Monroe na rapper Colonel Mustafa wa Kenya inazidi kuwa kubwa baada ya muimbaji wa Mombasa, Nyota Ndogo naye kuingia kwenye picha.clip_image003Nyoto Ndogo amempa makavu live rapper huyo wa Ogopa Deejays kuwa anachokifanya kinamshushia hadhi yake.

“Unayoyafanya unafkiria kuitwa baba kesho? maana ni upuuzi mtupu,” Nyota Ndogo amemchana Mustafa.

“Umri wako hauambatani na vituko unavyo vifanya kwahivyo rudi nyuma ubadilishe. shame on you. wewe hufai kuitwa kioo.clip_image003Umeshindwa kuandika nyimbo? kwaivyo unaona bora utafute visangaa? vinakupa sifa but unapata nini zaidi ya sifa hizo? hela kitandani?”

“Huyu mustafa hafai kuitwa kioo chajamii kabisa, umri wake na vituko vyake tafauti kabisa.uzee unaingia bado afanya mambo ya kitoto.shame,” aliongeza.

Mustafa na Huddah wameendelea kulianika penzi lao hadharani na hivi karibuni wataachia wimbo wao. “Can’t wait for my Song with @Mustafa_254 to land these streets . It was a first for me . But in life everything is possible,” alitweet Nyota Ndogo.

Post a Comment

Hii ni Blog kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Nchi yetu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...

Previous Post Next Post