Hatimaye sasa joto laanza kutanda kwa mashabiki wa soka mkoa wa lindi ikiwa imebakia siku moja kabda ya watani wa jadi hawajakutana.Nikiwa ninazunguka huku na kule kukusanya maoni juu ya mchezo huo. kila mtu akizungumzia kwa mtazamo wake lakini wengi wakiipa nafasi kubwa timu ya kusini Soccer fc kuweza kuibuka na ushindi hapo kesho kutokana na uwezo wakuweza kuuchezea mpira pamoja na kuwa na damu changa.
Timu hizo zilitoka sare ya kufungana goli 1-1 katika raund ya kwanza huku Kariakoo fc akiwa kama uwanja wa nyumbani, mechi ya kesho Kusini Soccer fc ndiye hatakaye kuwa nyumbani.Niliweza kuzungumza na kocha wa makipa wa kusini soccer fc MOHAMED SALAMATA (mudy m'bovu). Akisema wao kwa upande wao wamejianda vizuli kwa ajili ya mchezo huo na amesema kwajinsi walivyojianda wanaasilimia kubwa ya kuibuka na ushindi katika mechi hiyo.
Akiendelea alisema hawatoweza kufanya makosa ambayo yaliweza kuwaghalimu katika mechi zilizipita. Akimalizia huku kwa kuwapa moyo mashabiki wake kwa kusema waje kwa wingi kupata burudani mzuri kutoka kwa wachezaji wake.Je waamuzi hawa wataweza kuwapa wapenzi wa soka Iman ya Kuweza kukubaliana na Matokeo yatakayoweza kujitokeza?
Akika siku ya kesho apatoshi mjini lindi KUSINI SOCCER FC & KARIAKOO FC ndio habari ya mjini