HATIMAYE SASA HATI YA KUKAMATWA KWA RAIS YATOLEA RASMI!!

clip_image001Rais wa Ukraine aliyeondolewa madarakani Victor Yanukovych amefunguliwa mashtaka

Ukraine imetoa hati ya kukamatwa kwa Rais aliyeondolewa madarakani, Victor Yanukovych, Waziri wa mambo ya ndani wa mpito ametangaza hatua hiyo.

Arsen Avakov amesema katika ukurasa wa Facebook amesema kesi dhidi yake imefunguliwa dhidi ya Yanukovych na maafisa wengine kuhusu mauaji ya makubwa ya watu.

Wabunge walipiga kura kumuondoa Yanukovych siku ya jumamosi baada ya maandamano ya miezi kadhaa yaliyojitokeza baada ya kupinga kujiunga na Umoja wa Ulaya.

Machafuko yaliyotokana na maandamano hayo yalisababisha watu kadhaa kupoteza maisha juma lililopita.

Avakov amesema Yanukovych alionekana mjini Balaklava siku ya jumapili, lakini mpaka sasa hajulikani mahali alipo.

Post a Comment

Hii ni Blog kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Nchi yetu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...

Previous Post Next Post