Unknown Unknown Author
Title: CHELSEA OUT FA, SUNDERLAND IKIWA TIMU YA KWANZA KUINGIA ROBO FAINAL, WIGAN NAO WAPETA.
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Craig Gardner Akishangilia Mara Baada ya Kufunga Goli na Kuipeleka Timu yake ya Sunderland Robofainal ya Kombe la FA Sunderland ikifunga bao...

clip_image001Craig Gardner Akishangilia Mara Baada ya Kufunga Goli na Kuipeleka Timu yake ya Sunderland Robofainal ya Kombe la FAclip_image001[5]Sunderland ikifunga bao lake pekee dhidi ya Southampton

SUNDERLAND imeendelea kuonyesha maajabu baada ya kuwa klabu ya kwanza kutinga hatua ya Robo Fainali ya Michuano ya FA baada ya kuitandika Southampton kwa bao 1-0 katika pambano lililochezwa mapema leo.

Vijana hao wa Gustav Poyet waliokuwa wakichechemea kwenye  Ligi Kuu ya England, tayari imeshatinga fainali ya Kombe la Ligi (Capital One) itakapoumana na Manchester City mwezi ujao na ushindi huo wa leo umeipa uhakika wa kuendelea kuonyesha maajabu chini ya kocha huyo.

Bao lililoizamisha Southampton katika pambano hilo lililochezwa kwenye uwanja wa Light (Stadium of Light) liliwekwa kimiani katika kipindi cha pili na Craig Gardner.

Gardner alifunga bao hilo katika dakika ya 49 na kuipa wakati mgumu wageni wao kutafuta bao la kusawazisha lakini dakika 90 zilipoisha wenyeji walikuwa washindi na kutangulia robo fainali.

Cardiff 1 – 2 Wigan

clip_image001[7]Usiku huu Pia Timu ya Cardiff City Imemenyana na Wigan Athletic na Matokeo yake kuisha kwa Wigan Athletic Kuibuka Mshindi kwa Magoli 2 –1. Goli la Kwanza lilifungwa na Kiungo Chris McCann Kabla ya Campbell kusawazisha Goli hilo na Kufanya Matokeo kuwa 1 – 1,

mpiraNi Ben Watsona Ambaye alifunga goli la Ushindi wakati wa Mechi ya Fainali ya Kombe hilo Mwaka jana dhidi ya Manchester City kutoka yard 30 leo tena ameifungia timu yake goli muhimu lililoipa ushindi timu ya Wigan kwa kupiga free kick nzuri na kumshinda mlinda mlango na kujaa kimiani na kufanya matokeo kuwa 2 – 1.mpira 2

MANCHESTER CITY 2 - 0 CHELSEAclip_image001[9]Stevan Jovetic (katikati) akiifungia timu yake ya Manchester City goli la kwanza dhidi ya Chelsea katika Kombe la FA leo hii.

Manchester City imeikaribisha timy ya Chelsea na Kutolewa nje ya mashindano hayo kwa kuchapwa magoli 2 – 0. Manchester City wamekuwa wa kwanza kuzifumania Nyavu za Wenyeji wao kupitima mshambuliaji wa Stevan Jovetic.clip_image001[11]Hadi mapumziko Chelsea walikuwa nyuma kwa Goli hilo Moja na Kipindi cha pili kilianza kwa Kasi na Mchezaji Eden Hazard alijituma vilivyo kutafuta goli la kusawazisha lakini bila ya mafanikio waweza ona Katika Picha hapo chini jinsi gani alivyotembea uwanjani humo leo hiiclip_image001[13]Timu zote ziliweza kufaya marekebisho: Chelsea wao walimtoa Remires na Kumuingiza Mshambuliaji wao Frenando Torres na Manchester City wwalimtoa mfungaji wao wa goli la Kwanza Jovetic na Kumuingiza Samir Nasri akitoka katika Majeruhi.clip_image001[15]Kocha Pellegrin wa Manchester City ndio aliibuka na Ushindi katika Sub aliyoifanya kwani ilimsaidia kwa Mchezaji huyo kuifungia Bao la Pili na La Ushindi timu hiyo ya Manchester City na kuitoa nje Timu ya Kocha Jose Mourinho  katika kombe hilo la FA kwa Jumla ya Magoli 2 – 0.clip_image001[17]

About Author

Advertisement

Post a Comment Blogger

Toa Maoni Yako Kuhusu habari Hii

Note: Only a member of this blog may post a comment.

 
Top