Unknown Unknown Author
Title: BEN POL AJIPANGA KUUZA NYIMBO ZAKE KIDIGITALI ZAIDI
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Hitmaker wa Jikubali, Ben Pol amesema muda umefika kwake kuuza muziki wake kidijitali zaidi. Ben Pol ambaye anatarajia kuachia wimbo wake m...

clip_image001[9]Hitmaker wa Jikubali, Ben Pol amesema muda umefika kwake kuuza muziki wake kidijitali zaidi.

Ben Pol ambaye anatarajia kuachia wimbo wake mpya, Unanichora, mwezi huu amesema nyimbo zitakazofuata zitapatikana katika mitandao ya kibiashara kama Amazon,iTunes,Shazam,Google play,Beatsmusic,Xbox Music na Spotify.clip_image001

“Nimefanya hivi ili kuwaridhisha wale mashabiki ambao wanataka kuniunga mkono,” Ben ameaimbia Bongo5.

“Unajua wasanii kila siku tunalalamika tunaibiwa sijui hatupati maslahi ya muziki wetu,lakini pia kuna sehemu za watu ambao wanataka kununua. Mimi nyimbo zangu mfululizo nilikuwa natoa bure watu wa download wengi ili na mimi nione nyimbo yangu imesambaa nafanya show.Lakini kuna watu ambao hicho kitu kinawakera, nyimbo wanazipata lakini wanataka kununua. Watu wanasema ‘muziki wako una hadhi ya kununuliwa sio kupata bure sawa basi ni download bure basi nataka kununua ili na mimi nichangie’.

Kwasababu wanajua tunafanya maandalizi ya muziki huu kwa pesa. Kwahiyo nyimbo zangu zote nitakazotoa zitakuwa kwa mtindo huo. Media zote zitapata bure na kutakuwa na link za kusikiliza.”

Katika hatua nyingine, Ben Pol amesema wimbo wake mpya wa ‘Unanichora’ unazungumzia matukio kwenye mapenzi ambayo bado yanaendelea kutokea kwenye jamii.

Unanichora unazungumziA mapenzi yalivyobadilika siku hizi. Zamani ulikuwa wewe na mpenzi wako mnaheshimiana, mnatunziana siri mpaka wote mtakapoamua sasa hivi tukatambulishane kwa wazazi lakini sasa hivi yamekuwa kinyume,kila mtu anakaa kwa maslahi yake yaani mnachorana. Ndio maana ya wimbo, kitu ambacho hata mimi kimewahi kunitokea katika maisha ya mapenzi.”

About Author

Advertisement

Post a Comment Blogger

Toa Maoni Yako Kuhusu habari Hii

Note: Only a member of this blog may post a comment.

 
Top