Kampuni hiyo ya mtandao wa kijamii iliingiza mapato ya zaidi ya dola bilioni 2.5 katika robo tatu ya mwaka 2013.
Facebook ilianzishwa, tarehe 4, February 2004 na Mark Zuckerberg pamoja na wenzake waliokuwa wakisoma pamoja kwenye chuo kikuu cha Harvard ambao ni pamoja na Eduardo Saverin, Andrew McCollum, Dustin Moskovitz na Chris Hughes.
Hadi September mwaka jana, Facebook ilikuwa na watumiaji zaidi ya bilioni 1.2 duniani kote.
Je wewe Ulisherekeaje ukiwa ni miongoni mwa watu zaidi ya Bilioni 1.2 katika hii dunia, Hebu tueleze au ulipitwa bila kujua?
Tags
MAKALA