Mimi ni mtanzania ninaeishi swaziland katika mji wa MPAKA niko hapa toka mwaka 89 nimeoa na nina watoto wanne kwa mke wangu ambaye kwa kabila ni mngwane, kabila hili (japo si yote) lina mila na desturi zake ikiwamo hii ambayo wanaamin huwasaidia mabinti zao kuwa mbali na matendo yahusuyo ngono na wakifanikiwa kwa hilo binti anaechumbiwa au kuolewa anaonekana shujaa na familia anayotoka uthaminiwa sana. Mwanzo kwangu hili zoezi lilioneka gumu sana lakini toka nimuozeshe binti yangu aliyemaliza chuo kikuu guateng south afrika imenipa hari kubwa sana ya kudumisha huu utamaduni hapa nyumbani tz.
Kutokana na matatizo ya kifamilia ikiwamo misiba ilinilazimu nije na familia yangu yote mosi kuhani misiba na pili ni kutumia fursa hiyo kutambulishana kifamilia kwani ni kitambo hatujaonana lakini kinachonishangaza ni kuwa toka nifike hapa nyumbani (itumba) nimekuwa nikipokea shtuma toka kwa majiran kuwa kitendo anachowafanyia mke wangu kuwakagua watoto wetu si cha kiubinadam ikizingatiwa watoto ni wakubwa na wamekwisha vunjo ungo ingawaje nimepata taarifa hivi punde kuwa kati yao mmoja wao si salama kwani kipimo kinaonyesha 'kimepitiliza'
Nina mwezi mmoja tu wa kuwepo hapa na kama si bahati mbaya basi huenda nikapoteza kabisa sifa ya mabinti zangu kwani pande king mswati wamekuwa lulu, nimejenga nyumba nimenunua gari na sasa nategemea kusomesha watoto wa dadaangu marehemu na hilo litafanikiwa tu nikirudi na familia yangu salama pande zile za MPAKA swaz kwani tz ya sasa si ya kipindi kile majungu umbea vijana wamekalia vijiwe tu kupiga domo.
Ushauri wangu kwenu na hasa nyie vijana waleeni watoto wenu katika mfumo huo wa 'kaunta attack' kwani dunia ya sasa imearibika.
UMKIMTUNZA VYEMA ATAKUTUNZA VYEMA
Post a Comment Blogger Facebook
Toa Maoni Yako Kuhusu habari Hii
Note: Only a member of this blog may post a comment.