Unknown Unknown Author
Title: SHULE 4 ZA MKOA WA LINDI ZAKOSA WANAFUNZI WA KIDATO CHA KWANZA KWA MWAKA 2014
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Na Abdulaziz Lindi Shule Nne za kata kati ya shule 115 za sekondari zilizopo mkoani Lindi zimekosa wanafunzi wa kidato cha kwanza 2014 kutok...

clip_image003Na Abdulaziz Lindi
Shule Nne za kata kati ya shule 115 za sekondari zilizopo mkoani
Lindi zimekosa wanafunzi wa kidato cha kwanza 2014 kutokana na kukosa wanafunzi wa kujiunga na shule hizo.

Hayo yameelezwa na Afisa elimu wa mkoa wa Lindi Silas Samaluku wakati alipokuwa anatoa taarifa ya maendeleo kwa wajumbe wa kikao cha wadau wa elimu Mkoani Lindi.

Samaluku alisema kuwa Mkoa wa lindi una jumla ya shule za sekondari
115 na wanategemea wanafunzi wote waliofaulu watajiunga katika na
shule hizo lakini shule nne za sekondari kati ya hizo Namapwia na
Kilimarondo za wilayani Nachingwea, Madangwa wilayani Lindi na Nandanga wilayani Kilwa zitakuwa hazina wanafunzi wa kuanza kidato cha kwanza 2014 kutokana na kukosa wanafunzi wa kujiunga na shule hizo.

Alieleza kuwa wanafunzi 17,249 walisajiliwa kuhitimu elimu ya msingi
kati ya hao wavulana ni 7,981 na wasichana 9,448 lakini kati yao
waliofanya mtihani ni 16,682 na wasichana 9,150 sawa na asilimia
95.71.

Wanafunzi waliofaulu na kupata alama 100 hadi 250 walikuwa 6,857 kati ya hao wavulana 3,644 na wasichana 3,213 sawa na asilimia 41.1
ambayo imepanda ukilinganishwa na mwaka 2012 ambapo ilikuwa asilimia 22.60 .

Aidha Samaluku alibainisha kuwa kipindi cha miaka miwili mfululizo
wanafunzi wa wilaya ya liwale wanaongoza kwa kufanya vizuri mitihani ya darasa la saba kwa kushika nafasi ya kwanza kimkoa.

"mwaka 2013 Liwale imeongoza kwa kufaulisha kwa asilimia 53.37
ikifuatiwa na wilaya ya Nachingea kwa asilimia 50.05, Lindi manispaa
kwa asilimia 42.42 wilaya ya Ruangwa kwa asilimia 42.34, Kilwa
asilimia 33.74, wakati huo Lindi vijijini ikiendelea kushika mkia kwa
muda wa miaka miwili mfululizo kwa kuwa ya mwisho kupata asilimia 31.45

About Author

Advertisement

Post a Comment Blogger

Toa Maoni Yako Kuhusu habari Hii

Note: Only a member of this blog may post a comment.

 
Top