Unknown Unknown Author
Title: MADIWANI KILWA WAPITISHA BAJETI YA TSH 28,729,895,535 KWA MWAKA 2013/2014
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Madiwani wakiwa katika kikao cha kupitisha bajeti kinachoendelea katika ukumbi wa Jumba la maendeleo wilayani Kilwa Afisa Mipango wa Halmash...

DSC_0032Madiwani wakiwa katika kikao cha kupitisha bajeti kinachoendelea katika ukumbi wa Jumba la maendeleo wilayani KilwaDSC_0001Afisa Mipango wa Halmashauri ya wilaya ya kilwa, Daniel Lusingu akiwasilisha makisio ya bajeti ya Halmashauri hiyoDSC_0341 - Copy - Copy (2)Wakuu wa Idara wa Halmashauri wakihudhuria kikao hicho

ABDULAZIZ ,Kilwa
Halmashauri ya wilaya ya Kilwa imeomba kuidhinishiwa jumla ya Tshs
28,729,895,535 kwa ajili ya Uendeshaji wa shughuli mbalimbali za
serikali ikiwemo Mishahara Tshs 14,016,723,484 huku mapato ya ndani
ni Tshs 268,112,400 na matumizi mengineyo (OC) ni 1,567,578,000 toka serikali kuu na mapato ya ndani 2,054,184,359.

Aidha Miradi ya maendeleo tshs 2,994,804,988 toka serikali kuu na
wahisani 409,817.075 na mapato ya ndani Tshs 10,823,297,292.

Akisoma bajeti hiyo katika kikao cha Baraza maalum la bajeti kwa
Madiwani wa Halmashauri hiyo, Afisa Mipango wa Halmashauri ya wilaya ya Kilwa, Daniel Lusingu alibainisha kuwa Bajeti hiyo ina ongezeko la jumla ya Tshs 8.866,528,435 sawa na asilimia 44.63 ya bajeti ya mwaka 2013/2014.

Pamoja na maombi hayo ya kuidhinishiwa mapato na matumizi, Halmashauri ya wilaya ya Kilwa katika kuhakikisha inaongeza mapato kutoka katika vyanzo vya ndani imejipanga kuongeza wigo baada ya kubuni vyanzo vipya ikiwemo kuongeza wigo wa ukusanyaji kodi mbalimbali, Kuimarisha Uagizaji na utunzaji wa nyaraka za kukusanyia mapato na kuimarisha rejesta ya vyanzo vya mapato.

Sambamba na kuongeza wigo wa ubinafsishaji wa vyanzo na kufanya
uhakiki kila mara pamoja na kutoa elimu kwa walipa kodi na kuongeza
nguvu kwenye kudhibiti mazao yatokanayo na bahari, kilimo na misitu kwa kusimamia kwa karibu vizuizi katika maeneo ya Singino, Migeregere, Mbwemkuru, mihangalaya na Nanjirinji.

Akichangia bajeti hiyo, Diwani wa kata ya Songosongo, Mhe Hassan Swaleh pamoja na kuunga mkono Bajeti hiyo aliiomba Halmashauri hiyo kuona umuhimu wa kuthamini wavuvi kwa kupatiwa zana bora za uvuvi Ili kuongeza wigo katika makusanyo ya baharini

About Author

Advertisement

Post a Comment Blogger

Toa Maoni Yako Kuhusu habari Hii

Note: Only a member of this blog may post a comment.

 
Top