Watoto wa wili, Shaniya na Ally wa Moshi, wamekabidhiwa mkwanja wao, baada ya kushinda shindano la Pozi Kwa Pozi lililoandwaliwa na Ommy Dimpoz.
Picha iliyowapa ushindi Shaniya na Ally walioshinda shilingi laki tatu
Katika shindano hilo Ommy aliwataka mashabiki wamtumie picha wakiwa katika mapozi mbalimbali mshindi kujishindia shilingi laki 3. Ommy amesema katika shindano lijalo atatoa zawadi ya shilingi milioni 1.
Shaniya na Ally baada ya kupewa chao
Kwenye picha hiyo Ommy ameandika: Washindi wetu wa #pkp #pozkwapoz #laki3 ambao ni mtu na nduguye Shaniya na Ally wakiwa kwenye mapozi na Mpunga wao baada ya kuwafikia ni wakazi wa moshi….Mashaallaah Mungu Awajaalie Waendelee kupendana Inshaallaah tukutane tena kwenye Milioni moja Andaa kabisa Mapozi.”
Post a Comment Blogger Facebook
Toa Maoni Yako Kuhusu habari Hii
Note: Only a member of this blog may post a comment.