NAIBU WAZIRI WA HABARI,MH. JUMA NKAMIA ALIVYOPOKELEWA KATIKA OFISI ZA WIZARA HIYO LEO

clip_image001Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Prof. Elisante Olegabriel akimkaribisha Naibu Waziri wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Mheshimiwa Juma Nkamia katika tukio la kumkaribisha lililofanyika jijini Dar es Salaam leo.Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Utangazaji Tanzania Bwana Clement Mshana (kushoto) akimpongeza Mheshimiwa Naibu Waziri wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Mheshimiwa Juma Nkamia wakati wa mapokezi yake katika Ofisi za Wizara zilizopo jijini Dar es Salaam leo katikati ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara Prof. Elisante Olegabriel.Naibu Waziri wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Mheshimiwa Juma Nkamia akisalimiana na Kaimu Mkuu wa Kitengo cha TEHAMA Bwana Kulwa Magingila wakati wa mapokezi yake yaliyofanyika jijini Dar es Salaam leo kushoto ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara Prof Elisante Olegabriel.

Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Mheshimiwa Dkt. Fennela Mukangara akimkaribisha Naibu Waziri Mheshimiwa Juma Nkamia katika Ofisi za Wizara zilizopo katika jengo la Mfuko wa Pensheni wa PSPF jijini Dar es Salaam leo.Naibu Waziri wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Mheshimiwa Juma Nkamia akiongea na Wanahabari Ofisini kwake katika tukio la kumkaribisha lililofanyika jijini Dar es Salaam leo kulia ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara Prof Elisante Olegabriel.

Picha na Benjamin Sawe.

Post a Comment

Hii ni Blog kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Nchi yetu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...

Previous Post Next Post