Leo napenda kuleta Mjadala huu ilimradi tuweze kuwekana sawa katika hili la Wazazi wengi kupenda kulala na watoto wao katika Chumba kimoja bila kujali umri wa mtoto huyo kuwa unamfaa kuendelea kulala humo tangu azaliwe au la…
Hili jambo linatokea sana katika familia zetu za kiswahili hasa kwa wale ambao hawana kipato kikubwa cha kuweza kuandaa chumba maalum kwa ajili ya mtoto huamua kuweka kitanda kidogo ndani ya chumba cha baba na mama na kumtunza mtoto huyo humo hadi pale wazazi hao watakapoona inafaa kumuacha kulala peke yake au na Dada/Kaka zake.
Hapo Ndipo kwenye Shida kwani kuna wengine tunawaona mtoto ameshaanza darasa la kwanza lakini bado analala chumba cha Baba na mama ukitazama umri wa mtoto huyo ni Kuanzia Miaka 7 na Kuendelea ambaye kwa watoto wa siku hizi tayari ameshatambua zuri na baya..
Nakama tujuavyo chumbani kuna mengi hufanyika ambayo Mtoto hapaswi kuona katika kipindi hicho cha umri huo.
Je ndugu msomaji hebu tupe experience yako katika Hili……
Post a Comment Blogger Facebook
Toa Maoni Yako Kuhusu habari Hii
Note: Only a member of this blog may post a comment.