Mchezo wa Mwisho wa ligi daraja la Tatu wazidi kuwa kizungumkuti baaada ya Kuahirishwa kwa mara ya pili leo hii huku sababu zikitajwa kuingiliwa na Sherehe ya Dini ya Kiislam ya Maulidi ambayo inasomwa leo Usiku.
Akizungumza na blog hii Afisa Tawala wa TFF wilaya ya Lindi Ndg Ally Mkadeba ameeleza sababu hizo za kuahirishwa kwa mechi hiyo kwa siku hii ya leo na kusema mechi hiyo itachezwa Hapo kesho majira ya Saa 4:00 EAT jioni Ndani ya Uwanja wa Ilulu.
Ameongeza kuwa Mzunguko unaofuata utakuwa na mechi za Nyumbani na ugenini hivyo kwa wale watao fanikiwa kuingia katika hatua hiyo watakuwa na mechi mbili kwa kila timu pinzani tofauti na Mwakajana.
Hivyo Timu za Kariakoo fc na Kusini Soccer ambazo zitacheza mchezo wa mwisho hapo Kesho zitakuwa zote zimeingia katika hatua hiyo inayofuata lakini mchezo huo wa kesho utaamua nani mshindi wa kwanza na wapili katika msimamo wa ligi.
MTU ALIYEPOTEA APATIKANA NA KUTOA MAELEZO
Katika hali ya kustaajabisha mapema leo asubuhi habari zilitapakaa mjini hapa zikisemekana Mtu mmoja ambaye ni MGANGA wa kienyeji amepotea na kutekwa, Mtu huyo amepatikana na kusema ni kweli alichukuliwa na watu asio wajua kwa majina na Kumpeleka sehemu kusikojulikana..
Timu ya Kariakoo fc imekanusha tuhuma hizo za kuwa mtu huyo ni Mganga wao na kusema kuwa huyo ni shabiki wa Timu hiyo Tu na alikuja kuangalia mchezo ambao uliahirishwa hapo jana kutokana na Mvua kubwa iliyonyesha hapo jana.
Watu ambao hadi sasa wanao shikiliwa na Polisi kwa tuhuma hizo ni Khalfani Yahaya (KATIBU MSAIDIZI KUSINI SOCCER), Aguto (MJUMBE KAMATI KUSINI SOCCER) Bendi (dereva bajaji) Jovin Magali (KATIBU KARIAKOO FC)