LIGI DARAJA LA TATU NGAZI YA MKOA MKOANI LINDI:: KARIAKOO FC Vs KUSINI SOCCER LIVE AT ILULU STADIUM

LINDI derby

Leo Ndani ya Uwanja wa Ilulu Kutakuwa na Mpambano wa Kukata Na Shoka Katika Muendelezo wa Kuwania nafasi ya Mkoa Katika Ligi daraja La tatu Ngazi ya Mkoa:

Wengi wana Sema leo Ni Lindi Derby:: Ni kati ya Timu Mbili zenye Ushindani Mkubwa, Kariakoo Fc inaingia uwanjani ikiwa na Historia ya Kumfunga Kusini Soccer mara Moja na Kutoka nae droo moja katika Michezo miwili iliyochezwa Katika Hatua ya mwanzo. Kariakoo Fc imesha cheza Mechi Moja ya Ugenini na kushinda goli 2 - 1 dhidi ya timu ya Wilaya ya Nachinggwea hivyo kuwa na Point 3 hadi sasa.

Kusini Soccer itashuka dimbani kutafuta Point 3 na kufuta kuwa Mteja wa kariakoo kwa kutokuruhusu kufungwa kama ilivyotokea mechi za Awali, Pia nao wamesha cheza mchezo mmoja wa Ugenini dhidi ya Timu ya Wilaya ya Kilwa na Kushinda Goli 3 - 0 hivyo kufanya nao kuwa na point 3.

Basi Kama Uko Karibu Usipitwe na Mechi Hii Leo Saa Kumi Kamili Jioni Ndani ya Uwanja wa ILULU,

KARIAKOO FC Vs KUSINI SOCCER

Post a Comment

Hii ni Blog kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Nchi yetu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...

Previous Post Next Post