Kama ulivyokuwa katika Mchezo wao wa Awali Timu Hizi zenye Upinzani mkubwa Mjini Lindi Leo hii zimetoshana Nguvu katika mchezo wao wa Pili katika kutafuta Bingwa wa mkoa wa lindi..
Mechi hii haikuwa Na Tension Sana kwa mashabiki hata kwa Wachezaji leo hii kinyume na matarajio ya wengi kwani Mchezo ulichezwa kwa umakini na Rafu za hapa na Pale zilipungua ukilinganisha na Mchezo uliopita ambao walicheza na Kariakoo Kuibuka mshindi na kufanikiwa kuwa mshindi wa Kwanza katika kuongoza Ligi.Mpira Ulianza kwa Timu zote mbili kushambuliana kwa zamu lakini Ngome zote zilionesha uimara wao kwa Kuzuia hatari zilizokuwa zinajitokeza langoni mwao.
Dakika ya 38 ya mchezo Timu ya Kariakoo FC walipata Penalt kutokana na Beki wa Kusini Soccer Kumshika Mshambuliaji wa Kariakoo Hivyo Refa alilidhika na Faulo hiyo na Kuamuru Mkwaju wa Penalt ambayo iliwekwa Wavuni na mchezaji William Pilot na kuiandikia Bao la Kwanza la kuongoza.Baada ya Kariakoo Kupata goli Kusini Soccer ilizinduka na Kuacha Mchezo wao wa Kupiga Chenga badala ya kutafuta magoli, Kwa Mabadiliko hayo walifanikiwa nao Kupata Penalt Mnamo dakika ya 42 na iliwekwa wavuni na Mchezaji wao Mwalami Issa.
Kipindi cha Kwanza kilimalizika kwa timu hizo kutoka suluhu ya bao 1 – 1.Kipindi cha Pili hakikua Kizuri sana kimchezo kwani Timu zote mbili zilicheza mpira mbovu ambao haukuzinufaisha timu hizo huku Maamuzi ya waamuzi yakiwakera mashabiki waliohudhuria Mchezo huo kwani Dhahiri ilionesha kuwa walikuwa na Mapenzi katika Timu hizo.
Hadi mwisho wa mchezo Matokeo yalibakia kuwa 1 – 1.
Timu hizo Zitashuka Dimbani tena wiki ijao kwa Timu ya Kusini Soccer Kuikaribisha Generation Fc Kutoka Nachingwea
Post a Comment Blogger Facebook
Toa Maoni Yako Kuhusu habari Hii
Note: Only a member of this blog may post a comment.