TAFAKURI YANGU NA HISSAN SALUM
Nimesikitishwa na kushangazwa jinsi baadhi ya waandishi wa habari wanavoitumia vibaya karamu yao hasa waandishi wa habari za michezo!
Kocha Mkuu wa Young Africans: Hans Van Der Pluijm
Wanaufumba ukweli na kuandika uongo Kisa tu wametawaliwa na chuki dhidi ya uongozi wa timu fulani ni watu wa kuponda tu mradi ionekane uongozi fulani haufai!
Baada ya Jana kupost hapa kocha mpya wa YANGA wengi wamecomment Kuwa mzee hata inbox txt ni hizohizo,
Mbona tunakuwa wajinga wa kuamini asemalo mtu mmoja tu?mwaka Jana bayern munchen wamebeba treble ukiwa ni msimu wa mafanikio kwao, je yule kocha alikuwa na miaka mingapi?Sir Alex Ferguson anastaafu na kombe la ligii kuu uingereza je alikuwa na miaka mingapi?
Mnamkumbuka yule babu mfaransa wa simba aliyewapa nafasi hawa madogo ambao sasa simba inanufaika nao?alikuwa na miaka mingapi?kigezo cha kumponda huyu kocha eti mzee hakina mashiko!
Wengine wameenda mbali zaidi eti ana timuliwa timuliwa! klabu yake ya mwisho ni Medeama ya Ghana iliyokuwa inashirika confedaration cup. Na alijiuzulu alipoona mwenendo wa timu ni mbaya akiwa na mkataba wa miaka 2.
Nani hawajui mabingwa wa Ethiopia 2010 St George walivokuwa wanapiga mpira mzuri?nani asiyeijua berekuum Chelsea yaa Ghana ilivonyanya klabu bingwa Afrika, hearts of lions na medeama!
Nanukuu kauli ya makamu mwenyekiti wa Medeama ligi kuu Ghana akimtambulisha Hans van pluijm
"Napenda nimtambulishe Hans van pluijm Kuwa ndiye kocha mpya wa timu yetu, uzoefu wake, malengo, utendaji kazi wake ndio vigezo vilivompa nafasi!tunaamini mnamfahamu huyu kwa Kuwa alikuwa kocha na akaipa ubingwa st George, kocha wa Hearts of Lion, kocha wa Berkum Chelsea na sasa medeama analifahamu vilivo soka la Afrika tuna imani atatufikisha mbali katika michuano ya Afrika, naomba tumpe ushirikiano!
Sasa wewe mwenzangu na mimi hata hujui CV zake Kisa tu mwandishi fulani kaandika basi unakurupa na kuanza kuponda!Hapa wengine tayari washaanza mjengea mizengwe eti hafai!
Leo jioni atakuwepo kiwanjani kutazama fainali ya mapinduzi cup kati ya KCC na SIMBA SC kesho atakwea pipa kwenda uturuki kuungana na timu yake mpya!
KWELI MAISHA BILA UNAFIKI HAYAENDI
Karibu YANGA babu hans van der pluijm
Karibu Tanzania
GONGA LIKE KWA KOCHA MPYA YANGA