JE UMELIMISS KUNDI LA ECT?, HUU NDIO UJIO MPYA WA KUNDI HILO

Rapper, Gwamaka Kaihula aka King Crazy GK amewataka wapenzi wa East Coast Team kukaa mkao wa burudani baada ya members wa zamani wa kundi hilo AY na Mwana FA kumpa shavu kwenye Nyimbo zake kadhaa.clip_image001King Crazy GK amesema huu ni wakati wao wa kufanya kazi kama zamani kwa kutoa burudani nzuri ya muziki uliokwenda shule.

“Kwanza tumeanza kuongeza nguvu kwenye East Coast Team yetu mpya, sasa tunataka kama wanaume wawili na msichana mmoja. Pia Eastcoast Team ya zamani tumerudi tena pamoja na kuanza kufanya kazi pamoja. Tumeshaingia studio na kupika mambo kwahiyo hivi soon utawaona AY na FA na wengine ambao wlikuwa wanaunda Eastcoast Team ya zaman,” amesema GK.

“Tutatumia shule zetu kufanya muziki wenye ladha,” ameongeza. “Sasa hivi tunatakiwa kufanya kitu kipya katika performance,tunataka kufanya vitu ambavyo watu hawataamini kama ni sisi. Unajua tunatakiwa kuwa kwenye level nyingine,sasa tukiwa kwenye ileile ina maana hakuna sababu yakurudi pamoja tena. GK wa sasa anapiga kinanda,anapiga gitaa, kwahiyo hii ni level nyingine.”

SOURCE: BONGO 5

Post a Comment

Hii ni Blog kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Nchi yetu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...

Previous Post Next Post