Na Demetrius Njimbwi na Alexander Mpeka, Jeshi la Polisi
Jeshi la Polisi Nchini limesema kuwa, litamchukulia hatua kali mtu ama kikundi chochote katika jamii chenye lengo la kutaka kuvunja, kuhatarisha amani au kuwa sehemu ya uhalifu jambo ambalo ni kinyume cha sheria za nchi.
Kauli hiyo imetolewa jana na kamishna wa Polisi Jamii Nchini (CP) Mussa Alli Mussa, wakati wa mkutano wa maofisa wa Polisi pamoja na askari wa vyeo mbalimbali uliofanyika katika mkoa wa kipolisi wa Kinondoni, jijini Dar es salaam.
Kamishna Mussa, alisema kuwa, kutokana na kupungua kwa matukio ya uhalifu na wahalifu, kumechangiwa zaidi na uelewa wa wananchi pamoja na kushiriki kwao katika dhana nzima ya Polisi Jamii/Ulinzi Shirikishi jambo ambalo kwa sasa limeifanya jamii kuishi kwa amani.
Hata hivyo, kamishna Mussa, aliwataka askari kuongeza ufanisi katika kuwahudumia wananchi ikiwa pamoja na kuwataka wananchi na wadau mbalimbali wa Polisi Jamii/Ulinzi Shirikishi kuendelea kushirikiana na Jeshi la Polisi pamoja na kufichua mitandao ya uhalifu.
Kwa upande wake Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) Lazaro Mambosasa, amewataka askari pamoja na watendaji wa Jeshi la Polisi kutokujitenga katika kueneza dhana ya Polisi jamii/Ulinzi shirikishi na badala yake wajikite zaidi katika kutoa huduma bora kwa wananchi ili kuisaidia jamii kuondokana na changamoto za matukio ya uhalifu na wahalifu.
About Author
JE, UNA HABARI, PICHA, TANGAZO, MAKALA NA USHAURI? USISITE KUWASILIANA NASI SIMU / WHATSAPP NAMBA 0625535420.
Advertisement
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Post a Comment Blogger Facebook
Toa Maoni Yako Kuhusu habari Hii
Note: Only a member of this blog may post a comment.