Mwaka jana zilifanyika fainali za shindano la kusaka vipaji lijulikanalo kama Epiq Bongo Star Search ambapo mshindi aliibuka Emmanuel Msuya na kujinyakulia kitita cha shilingi milioni hamsini.
Mara baada ya kuwa kimya tangu anyakue kitita hicho, leo hii Madam Ritha ambaye ndio mmiliki wa shindano hilo amepost picha mtandaoni ikionyesha gari aina ya Opa, Nyumba na Studio ndani yake akiwemo Emanuel huku post hiyo ikisindikizwa na maneno hayo hapo chini;“Gari, nyumba na studio ya Mshindi wa EBSS 2013 Emmanuel Msuya. Tayari Emmanuel ameshaanza kurekodi nyimbo za wasanii wengine kupitia studio yake na hivi karibuni anatarajia kuachia video ya wimbo wake na kazi zake nyingine.”
Post a Comment Blogger Facebook
Toa Maoni Yako Kuhusu habari Hii
Note: Only a member of this blog may post a comment.