Big Boss wa MayBach Music Group Rick Ross, amemwaga mamilioni ya dola kununua jumba la kifahari lenye vyumba 109 kwaajili ya makazi yake, ambayo kwa huku kwetu hiyo ni hotel kabisa tena kubwa tu.
Jumba hilo lililoko Atlanta, Georgia, Marekani hapo kabla lilikuwa likimilikiwa na bondia Evender Holyfield.Mansion hiyo yenye ukubwa wa 54,000 square feet ina kila kitu unachoweza kutamani kuwa nacho kwenye nyumba, ikiwa ni pamoja na swimming pool kubwa, home movie theatre, uwanja wa basetball, na dinning room yenye uwezo wa kuchukua watu 100 kwa pamoja.Haijawekwa wazi kiasi ambacho Rozay ametoa kununua mansion hiyo, lakini July,2012 Evender aliweka sokoni mjengo huo kwa dola milioni 14.Inasemekana gharama za kuendesha mjengo huo haipungui dola milioni 1 kwa mwaka, pamoja na bill za umeme zinazofika $17,000.
Post a Comment Blogger Facebook
Toa Maoni Yako Kuhusu habari Hii
Note: Only a member of this blog may post a comment.