FA CUP ndio Kombe la mwisho kwa Arsenal kutwaa tangu Mwaka 2005 na Ijumaa wao ndio wataanza kucheza Mechi za Raundi ya 4 wakiwa kwao Emirates na kupambana na Timu ya Daraja la chini Coventry.
Wenger ametamka: “Nilibahatika kulitwaa mara 4 lakini bahati mbaya hatujashinda kwa muda mrefu na sasa natilia mkazo kutwaa FA CUP.”
Hiyo Ijumaa pia ipo Mechi nyingine ya FA CUP kati ya Nottingham Forest na Preston na Jumamosi zipo Mechi 12 wakati Jumapili zipo Mechi mbili.
Kwa sababu ya Mechi hizi za FA CUP, Ligi Kuu England haitachezwa hadi Jumanne Januari 28 na Jumatano Januari 29.
Post a Comment Blogger Facebook
Toa Maoni Yako Kuhusu habari Hii
Note: Only a member of this blog may post a comment.