Unknown Unknown Author
Title: HII NAYO KALI: BABA MZAZI AMSHTAKI MWANAWE KWA KOSA LA KUOA MWANAMKE MASIKINI
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
PATNA, India  -- MWANAMUME nchini India amemshtaki mwanawe wa pekee wa kiume katika  mahakama kwa kumharibia sifa, alipoamua kumuoa mwanamke...

clip_image001PATNA, India  -- MWANAMUME nchini India amemshtaki mwanawe wa pekee wa kiume katika  mahakama kwa kumharibia sifa, alipoamua kumuoa mwanamke wa tabaka la  chini. Alisema kwamba kitendo hicho kimemharibia sifa na hadhi yake katika jamii.

Mzee  Sidhnath Sharma anataka alipwe rupia 10,000,000 (KSh13,638,900) na  mwanawe Sushant Jasu, na anataka mahakama iamuru kwamba kijana huyo  asitumie tena jina la familia.

Sharma, ambaye ni wakili kutoka ukoo wa familia ya watu wanaojiweza ya Bhumihar, alisema ndoa aliyofunga mwanawe mwishoni mwa  mwaka jana ilivunja mwiko ambao umedumishwa kwa miaka 400, kwamba mtu wa  familia ya hadhi ya juu hafai kumwoa wa walalahoi.

“Kwa  miaka mingi, sheria hii imekubaliwa na kwamba ndoa ni lazima zipangwe  na wazazi kwa sababu ya kuwa mtu amuoe wa hadhi yake. Lakini mwanangu  pekee ameamua kumaliza utamaduni huu. Sio tu kwamba nimepigwa na butwa,  bali pia kitendo chake kimetia doa hadhi yangi katika jamii,” aliambia  shirika la Habari la Ufaransa, AFO nyumbani kwake mjini Danapur,  viungani mwa jiji la Patna.

Mtindo huo wa  kuwagawa watu katika makundi kulingana na hadhi zao, umerithiwa mno  nchini India kiasi kwamba umekita mizizi hata miongoni mwa wasomi na  watetezi wa haki za binadamu.

Cha kushangaza ni kwamba, unafuatwa hata katika jimbo la Bihar, mojawapo ya maeneo maskini zaidi na yenye idadi kubwa ya watu nchini India.

Itikadi  hiyo ndiyo dira hasa ya maisha ya watu wengi wa India, na inaweza  kuamua kuhusiana na masuala ya ndoa, elimu, ajira na umiliki wa ardhi,  japokuwa sharia za nchi hiyo zinapiga marufuku kuwabagua watu kwa  misingi ya hadhi zao.

Watu  wanaokwenda kinyume na wazazi wao na kuamua kuoa nje ya matabaka yao,  mara kwa mara wamekuwa wakiuawa, katika kinachotajwa kuwa 'mauaji ya  kuhifadhi hadhi’ ili wanandoa wasiharibu heshima na sifa za wazazi wao.  Sharma aliwasilisha keshi dhidi ya Jasu mwezi uliopita na mahakama mjini  Danapur inatarajiwa kuanza kuisikiza kesi hizo kesho Jumamosi.

Jasu,  ambaye ni afisa mkusanyaji mapato katika jimbo la Gujarat, alimwoa mke  huyo anayefanya kazi katika benki mjini Danapur mwezi Novemba mwaka  jana. Sharma anasema iwapo mwanawe ataendelea kutumia jina la familia  kwenye jina lake, ataomba alipwe rupia 10,000 kama ada ya hakimiliki,  kila mara atakapotajwa au kusikika akiitwa na mtu.

“Nimeiomba  mahakama imwagize anilipe kwa kuniumizahisia zangu, kisaikolojia na pia  kwa kuniharibia hadhi yangu katika jamii. Ninataka anilipe gharama  yangu yote niliyopata kumfanya awe mtu aliye sasa,” akasema. Jasu alikataa kuzungumza kuhusu kesi hiyo.

CHANZO: MPEKUZI

About Author

Advertisement

Post a Comment Blogger

Toa Maoni Yako Kuhusu habari Hii

Note: Only a member of this blog may post a comment.

 
Top