Hii leo huko Uingereza Magazeti yote yameweka Bango kubwa kuwa Staa wa Chelsea, Juan Mata, yuko mbioni kusaini Manchester United kwa Dau la Pauni Milioni 37 ambalo ni Rekodi kwa Mabingwa hao wa England.
Mchezaji huyo wa Spain, ambae hapangwi na Meneja wa Chelsea Jose Mourinho kwenye Kikosi chake, inadaiwa anataka kuhama ili kupata nafasi kubwa ya kucheza na hivyo kuchukuliwa na Mabingwa wa Dunia, Spain, kucheza Fainali za Kombe la Dunia huko Brazil Mwezi Juni.
Msimu huu Mata ameanza Mechi 11 tu za Ligi akiwa na Chelsea na tangu aonyeshe hasira alipobadilishwa kwenye Mechi dhidi ya Southampton hapo Januari Mosi, hajapangwa Mechi yeyote.
Mata, ambae ni Kiungo, amekuwa hana namba kwani Mourinho hupenda kuwachezesha Hazard, Oscar na Willian katikati nyuma ya Straika wao pekee.
Mata, ambae ameichezea Spain mara 32, alijiunga na Chelsea kutoka Valencia kwa Dau la Pauni Milioni 23.5 Mwezi Agosti 2011 na amekuwa akishinda Kura ya Mchezaji Bora wa Chelsea kwa Miaka miwili mfululizo iliyopita kwa kuiwezesha Klabu kutwaa FA CUP, UEFA CHAMPIONZ LIGI na EUROPA LIGI.
Ripoti za Magazeti ya huko Uingereza zimedai, Ofa rasmi ya Man Uunited itatolewa ndani ya Masaa 48.
Hata hivyo, si Chelsea wala Man United, hadi sasa, iliyoibuka kukiri au kukanusha habari hizi.
FA YAMSHITAKI NICOLAS ANELKA: KUHUSU SALUTI QUENELLE"!!Straika wa West Bromwich Albion, Nicola Anelka, amefunguliwa Mashitaka na FA, Chama cha Soka England, kwa kutumia Saluti iitwayo “Quenelle" ambayo inahusishwa na Mafashisti wa Nazi na Ubaguzi kwa Mayahudi.
Anelka, Miaka 34, alitoa Saluti hiyo ambayo Mkono mmoja unanyooshwa chini na mwingine kupita Kifuani na kuugusa mwingine, wakati alipofunga Bao kwenye Mechi na West Ham hapo Desemba 28.
Anelka alikabidhiwa Kabrasha la Kurasa 34 likielezea Tuhuma dhidi yake na amepewa hadi Saa 3 Usiku Januari 23 kujibu Tuhuma hizo.
Hapo Jana, Wadhamini wa West Brom, Zoopla, waliamua kuachana na Klabu hiyo mwishoni mwa Msimu kufuatia kitendo hicho cha Nicolas Anelka kutumia Saluti hiyo “Quenelle".
KIPA WA BRAZIL JULIO CESAR KUIHAMA QPR JANUARIMwenyekiti wa QPR Tony Fernandes ametoboa kuwa Kipa wao, Julio Cesar, ambae ndie Kipa Nambari Wani wa Brazil, ataihama Klabu yao Mwezi huu.
Cesar, Miaka 34, amechezea Mechi moja tu Msimu huu QPR walipofungwa 4-0 na Everton mwanzoni mwa Mwezi huu na huku Fainali za Kombe la Dunia zikichezwa Nchini Brazil kuanzia Juni 12, Kipa huyo mahiri anategemewa kuhama ili acheze mara kwa mara na kupata uhakika wa kuwemo Kikosi cha Brazil.
QPR walimchukua Kipa Rob Green ili kuziba pengo la Julio Cesar wakitegemea Mbrazil huyo kuhama mwanzoni mwa Msimu lakini hilo halikutokea lakini pia hilo liliwafanya QPR kumtumia Green badala ya Cesar.
Hivi sasa Klabu ya Italy, Cagliari, imeibuka kuwa ndio anakoelekea Kipa huyo.
SOURCE: SOKA IN BONGO
Post a Comment Blogger Facebook
Toa Maoni Yako Kuhusu habari Hii
Note: Only a member of this blog may post a comment.