KIUNGO wa Manchester United, Darren Fletcher, amesema Timu yao hainachochote cha kuogopa kwa tripu ya Jumapili huko Stamford Bridge kuivaa Chelsea kwenye Mechi ya Ligi Kuu England.Man United watatua Stamford Bridge wakiwa wametoka kwenye vichapo vitatu mfululizo tangu Mwaka mpya uanze na kisha kuichapa Swansea City Uwanjani Old Trafford katika Mechi yao ya mwisho ya Ligi.
Tofauti na wao, Chelsea wanapaa katika mbio za Ubingwa Msimu huu wakiwa wamekusanya Pointi 25 kati ya 30 katika Mechi zao 10 za mwisho za Ligi.
Muhimu zaidi kwa Chelsea ni ile Rekodi ya Jose Mourinho ya kutofungwa Uwanjani Stamford Bridge kwenye Ligi katika himaya zake zote mbili akiwa na Chelsea, ile ya Mwaka 2004 hadi 2007, na hii ya mara ya Pili.
Hata hivyo, Darren Fletcher, baada kurudi kwa kishindo Uwanjani kufuatia kupona kwake ugonjwa wa Tumbo uliomweka nje Mwaka mzima, amesisitiza Timu yao haina mchecheto na Mechi hiyo.
Ametamka: “Hapana, hata kidogo, sisi tunatarajiwa kushinda kila Mechi na haijali ni Swansea Nyumbani au Chelsea Ugenini. Ni maafa tusiposhinda!”
WAKATI HUO HUO, zipo taarifa kuwa Kiungo wa Man United kutoka Brazil, Anderson, yupo njiani kwenda Italy kupimwa afya na Klabu ya Fiorentina ili kuhamia huko ingawa pia inadaiwa ni kwa Mkopo.Anderson amedumu Old Trafford kwa Miaka 6 na Nusu na kucheza karibu Mechi 100 za Ligi.
Kuondoka huku kwa Anderson ni dalili kuwa David Moyes anakaribia kumsaini Kiungo mwingine ingawa hamna uthibitisho wowote.
RATIBA: LIGI KUU ENGLAND
| Jumamosi Januari 18 | Jumapili Januari 19 | ||
| SAA | TIMU ZINAZOCHEZA | SAA | TIMU ZINAZOCHEZA |
| 1545 | Sunderland v Southampton | 1630 | Swansea v Tottenham |
| 1800 | Arsenal v Fulham | 1900 | Chelsea v Man United |
| 1800 | Crystal Palace v Stoke |
| |
| 1800 | Man City v Cardiff | Jumatatu Januari 20 | |
| 1800 | Norwich v Hull | SAA | TIMU ZINAZOCHEZA |
| 1800 | West Ham v Newcastle | 2300 | West Brom v Everton |
| 2030 | Liverpool v Aston Villa |
|
|
| Jumanne Januari 28 | Jumatano Januari 29 | ||
| SAA | TIMU ZINAZOCHEZA | SAA | TIMU ZINAZOCHEZA |
| 2245 | Man Utd v Cardiff | 2245 | Aston Villa v West Brom |
| 2245 | Norwich v Newcastle | 2245 | Chelsea v West Ham |
| 2245 | Southampton v Arsenal | 2245 | Sunderland v Stoke |
| 2245 | Swansea v Fulham | 2245 | Tottenham v Man City |
| 2300 | Crystal Palace v Hull |
|
|
| 2300 | Liverpool v Everton |
|
|
MSIMAMO:
| NA | TIMU | P | GD | PTS |
| 1 | Arsenal | 21 | 22 | 48 |
| 2 | Man City | 21 | 36 | 47 |
| 3 | Chelsea | 21 | 21 | 46 |
| 4 | Liverpool | 21 | 25 | 42 |
| 5 | Everton | 21 | 15 | 41 |
| 6 | Tottenham | 21 | 1 | 40 |
| 7 | Man United | 21 | 11 | 37 |
| 8 | Newcastle | 21 | 2 | 33 |
| 9 | Southampton | 21 | 4 | 30 |
| 10 | Hull | 21 | -5 | 23 |
| 11 | Aston Villa | 21 | -7 | 23 |
| 12 | Stoke | 21 | -13 | 22 |
| 13 | Swansea | 21 | -4 | 21 |
| 14 | West Brom | 21 | -5 | 21 |
| 15 | Norwich | 21 | -18 | 20 |
| 16 | Fulham | 21 | -24 | 19 |
| 17 | West Ham | 21 | -10 | 18 |
| 18 | Cardiff | 21 | -18 | 18 |
| 19 | Sunderland | 21 | -15 | 17 |
| 20 | Crystal Palace | 21 | -18 | 17 |