Mwenge wa Jumuiya ya Madola (Queens Baton Relay) leo umetembelea Hospitali ya Taifa Muhimbili jumapili ukiongozwa na Mheshimiwa Balozi wa Uingereza nchini Tanzania Bi. Dianna Melrose pamoja na mshindi wa mbio za kilomita 1500 za jumuiya ya madola Bw. Filbert Bayi.
Mwenge huu umetembelea Hospitalini hapa kwa nia kubwa ya Kukutana na watoto wanaougua saratani mbalimbali ili kuwapa matumaini ya kuishi na kwamba jamii inawanathamini. Watoto hawa wamepata fursa ya kuushika mwenge huu na kupiga picha kama kumbukumbu muhimu katika maisha yao fuatulia katika picha jinsi watoto walivyofurahia mwenge huo.
Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili Dkt. Marina Njelekela akipokea mwenge kutoka kwa kiongozi wa michezo ya Olimpiki kutoka Kenya Bw. Kipchoge Keino
Dkt. Njelekela akimkabidhi mwenge mtoto anayeugua ugonjwa wa saratani.
Watoto wakiendelea kufurahia mwenge.
Watoto wakiendelea kufahia.
Muuguzi akiwa amemsaidia mtoto aliyelazwa wodini kushika mwenge.
Aliyechuchumaaa kutoka kushoto ni Balozi wa Uingereza nchini Tanzania Bi. Dianna Melrose akiwa na watoto katika mojawapo ya wodi za kulaza watoto.
Watoto wakishangilia kwa furaha pamoja na ujumbe wa mbio za mwenge wa jumuiya ya madola.
Mtoto aliyelazwa wodini akisaidiwa na muuguzi kuushika mwenge.

