That’s right…mapema siku ya jana, Januari 6, Diamond Platnumz aliachia ngoma yake, “My Number One” Remix ambayo ameshirikisha Davido all the way from Nigeria . Moja ya mstari aliouimba Davido kwenye ngoma hii ni kipisi kisemacho “Tanzania to Lagos”, kinachoashiria ushirikiano mzuri kati ya nchi hizi mbili, ila safari hii, Davido ameelekeza mashambulizi ya burudani pande za Uganda, kwa mkali Dr. Jose Chameleone.
Kupitia ukurasa wa Facebook wa nguli huyu wa muziki kutoka Uganda, anayetamba na kibao chake kiitwacho “Tubonge”, amewashirikisha wapenzi wa muziki na mashabiki wake furaha aliyokuwa nayo kwa kuona mwaka mpya na kudodosa kuwa kazi inayofuata atakuwa ameshirikiana na mkali huyo wa Naija, Davido.Si hilo tu, bali Chameleone ali share kipande kidogo cha audio ya jinsi mdundo huo utakavyoskika mara baada ya kutoka.
Post a Comment Blogger Facebook
Toa Maoni Yako Kuhusu habari Hii
Note: Only a member of this blog may post a comment.