CHELSEA WAMREJESHA NEMANJA MATIC KWA PAUNDI MILIONI 21

clip_image001[5]Kiungo raia wa Serbia Nemanja Matic amesajiliwa tena kwa mkataba wa miaka 5 na nusu.

clip_image001Chelsea imekamilisha uhamisho wa kiungo raia wa Serbia Nemanja Matic kutoka klabu ya Benfica ya Ureno.

Matic ambaye anarejea Chelsea baada ya kuihama akiwa ni sehemu ya uhamisho wa beki David Luiz,amesajiliwa tena kwa mkataba wa miaka 5 na nusu kwa ada ya uhamisho ya paundi milioni 21.

Kiungo huyo mwenye umri wa miaka 25 tayari amekabidhiwa jezi namba 21.

Post a Comment

Hii ni Blog kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Nchi yetu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...

Previous Post Next Post