Ujumbe wa Viongozi wa dini wakiangalia mojawapo ya visima vya nchi kavu vya kusafisha gesi katika eneo la Mnazi Bay, Mtwara.
Viongozi wa dini wametembelea Bomba Jipya la Gesi asilia la Mtwara- Dar es Salaam, mtambo wa kusafisha umeme wa Mnazi Bay na maeneo mengine mbalimbali ya uendelezaji wa gesi asilia katika Mkoa wa Lindi na Mtwara.
Viongozi hao wamefanya ziara hiyo ikiwa ni maandalizi kabla ya kufanyika Kongamano la Viongozi wa dini linalotarajiwa kufanyika jijini Dar es Salaam tarehe 21 na 22 mwezi Januari, 2014.Viongozi wa dini wakipata maelezo kutoka kwa Mtaalamu wa Masuala ya gesi na Msimamizi Mkuu wa Mitambo ya kusafisha gesi Mhandisi Sultan Pwaga katika eneo la Madimba kinapojengwa Kiwanda cha kutakasa Gesi.
Mafundi wa Kampuni ya China Petroleum Pipline (CPP) wakiendelea na kazi ya kuunganisha mambomba ya gesi katika kambi ya Madangwa.
Meneja Mradi wa Bomba la gesi kutoka Da r es Salaam hadi Mtwara Mhandisi Kapuulya Musomba akiwaeleza viongozi wa hatua mbalimbali zilizofikiwa katika utekelezaji wa Mradi huo. Katikati ni Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Nishati na Madini Mhandisi Ngosi Mwihava.