Unknown Unknown Author
Title: YOUNG KILLER ATABIRIWA MAKUBWA NA MMAREKANI..!! CHEKI HAPA
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Super ‘Nyota’ ya Young Killer Msodoki inazidi kung’aa, sio tu Tanzania bali hadi Marekani tayari ameanza kupata mashabiki. Shabiki mpya wa Y...

clip_image001Super ‘Nyota’ ya Young Killer Msodoki inazidi kung’aa, sio tu Tanzania bali hadi Marekani tayari ameanza kupata mashabiki. Shabiki mpya wa Young Killer ni mzungu mwenye umri mdogo pia kama yeye, ambaye amesema anamzimia Msodoki japo haelewi lugha ya Kiswahili lakini amejaribu kurap juu ya wimbo wake.

Shabiki huyo anayeitwa Stephen Tracy raia wa Marekani amejirekodi video akirap juu ya wimbo wa Young Killer msodoki na Stamina ‘Jana na Leo’, kisha akaiweka video hiyo youtube katika channel yake ikiwa na title ‘stephen. usa young killer songs’.Katika video hiyo (hapo juu) baada ya kujaribu kuifuata mistari ya Killer ambayo ilikuwa ikimshinda sababu hajui Kiswahili, baadae alizungumza na kumpa ujumbe (hapo chini) Young Killer.

“Young Killer, sikuwa nakufahamu lakini baada ya Junior kunielezea maana ya wimbo wako ninaupenda wimbo wako. Unaweza kuwa rapper mkubwa Marekani, na natamani nikutane na wewe, kama ungekuja Marekani ungetenegeneza pesa nyingi, na nyimbo zako Superstar na Stamina (akimaanisha Jana na Leo) zote ni nyimbo nzuri. So kama ukiendelea kurap utakuja kuwa mkubwa na mimi ni shabiki wako mkubwa.”

“Young Killer, I didn’t know you but after Junior explained to me what your song meant I love your song, you could be a big rapper in the USA , and I wish I can meet you and if you came to the US you could make a lot of money, and your song Superstar and Stamina they are both good songs, so If you keep rapping you will be big sometimes and your biggest fan.”

Hii ni ishara nzuri sana kwa Msodoki ambaye hana muda mrefu sana katika game lakini tayari ameshaanza kupata mashavu yanayodhihirisha kuwa uwezo wake ni mkubwa.

Msikilize hapa akimpa ujumbe Young Killer

ORIGINAL SOURCE: BONGO 5

About Author

Advertisement

Post a Comment Blogger

Toa Maoni Yako Kuhusu habari Hii

Note: Only a member of this blog may post a comment.

 
Top