Bado haki za marehemu Sharo Milionea zinazidi kumtesa mama yake mzazi, Zainabu Mkiety ambaye ameendelea kulalamika kuwa watu wanaopaswa kuzilipa wamejikausha!
Kwa mujibu wa Global Publishers, mama Sharo amesema watu ambao walikuwa wanadaiwa na Sharo kupitia kazi ambazo alizifanya wamenyamaza bila kumwambia nini kinachoendelea.
Mama Sharo amesema hakuna alichoambulia zaidi ya fedha za gari alilokuwa anatumia marehemu pamoja na vitu vya ndani.
“Nawaomba wasinidhulumu jamani, nahangaika na uzee huu, mwanangu alikuwa ndiye nguzo maishani mwangu, mfano niliona hadi kalenda lakini sikuona chochote juu ya kalenda hizo, nawaomba sana,” mama Sharo amemwambia mwandishi wa Global Publishers.
Post a Comment Blogger Facebook
Toa Maoni Yako Kuhusu habari Hii
Note: Only a member of this blog may post a comment.