Benchi la Timu ya Lindi Sports fc Iliyo chapwa goli moja katika Mchezo wake na Kariakoo Fc katika Ligi Daraja la Tatu.
Benchi la Ufundi la Timu ya Kariakoo Fc iliyocheza leo na Timu ya Lindi Sports katika mchezo wa Ligi daraja la tatu, ilishinda goli moja.
Wachezaji wa Timu ya Kariakoo Fc Wakishangilia Mara baada ya Kuifunga Timu ya Lindi Sports Bao moja katika Mchezo wa Ligi daraja la Tatu uliochezwa leo katika Uwanja wa Ilulu mjini Lindi
Mchezaaji wa Timu ya Kariakoo Fc akipandishwa Kwenye gari la Jeshi la kujenga Taifa kukimbizwa Hospitali ya Mkoa kwa Matibabu ya haraka mara baada ya kupigwa kiwiko na mchezaji mwenzake wa Lindi Sports. Mchezaji huyo alitolewa nje kwa Kadi nyekundu nakufanya timu hiyo kucheza pungufu hadi mwisho wa mchezo huo.
Golkipa wa Lindi Sports akilalamikia maamuzi ya Refarii kwa kushindwa kuwaadhibu wachezaji wa Timu ya Kariakoo Fc waliokuwa wakipigana uwanjani na badala yake kumwadhibu mchezaji mmoja tu wa timu yake, pia kushindwa kuwaadhibu benchi la ufundi la Kariakoo kwa kuingia uwanjani mara baada ya kutokea vurugu hizo tena mbaya zaidi ikiwa ni mashabiki na si kocha wala kiongozi wa timu.
Wachezaji wa Kariakoo wakitoka uwanjani mara baada ya dakika 45 za kipindi cha kwanza kumalizika na wakiwa mbele kwa goli moja.
Viongozi wa Chama cha Mpira wa miguu Mkoa wa Lindi wakifuatilia Mtanange huo kwa Umakini wa Hali ya Juu.
Wachezaji wakizongana Kuhusiana na Beki wa Kariakoo Kunawa mpira karibu na eneo la hatari na refa kuamuru kupikwa free kick kuelekea langoni mwao.
Washabiki wa Mji wa Lindi Wakiishangilia Timu ya Kariakoo Mara baada ya Refa Kupuliza kipenga cha mwisho kuashiria mpira umemalizika na Kariakoo Fc kuibuka Kidedea kwa kuchukua point Tatu muhimu na kujikita kileleni huku akifuatiwa na Timu ya Kusini Soccer iliyo shinda hapo jana.
Post a Comment Blogger Facebook
Toa Maoni Yako Kuhusu habari Hii
Note: Only a member of this blog may post a comment.