Bao la Kichwa la Olivier Giroud katika Dakika ya 65 leo limeifanya Arsenal iifunge Newcastle huko St James Park Bao 1-0 na kutwaa tena uongozi wa Ligi Kuu England wakiwa Pointi 1 mbele ya Manchester City.
Ingawa Arsenal walifungua nafasi kadhaa za kufunga lakini ni Newcastle waliokosa Bao za wazi wakati Shuti la Moussa Sissoko lilipookolewa na Kichwa cha Mathieu Debuchy kupiga posti.
Goli hilo la Arsenal lilipatikana baada ya Frikiki ya Theo Walcott kuunganishwa na Giroud.
Ushindi huu umewafanya Arsenal wawe kileleni mwa Ligi Kuu England Siku ya Mwaka mpya kwa mara ya kwanza tangu Msimu wa 2007/08.
VIKOSI: Newcastle: Krul, Debuchy, Coloccini, Williamson, Santon, Tiote, Anita, Sissoko, Cabaye, Gouffran, Remy
Akiba: Cisse, Ben Arfa, Yanga-Mbiwa, Haidara, Elliot, Shola Ameobi, Sammy Ameobi.
Arsenal: Szczesny, Sagna, Mertesacker, Koscielny, Gibbs, Flamini, Wilshere, Walcott, Cazorla, Rosicky, Giroud
Akiba: Arteta, Podolski, Fabianski, Bendtner, Jenkinson, Miyaichi, Gnabry.
Refa: Lee Probert (Wiltshire)
EVERTON 2 SOUTHAMPTON 1Mchezaji wa Mkopo kutoka Chelsea, Romelu Lukaku, leo Uwanjani Goodison Park ameifungia Bao la Pili na la ushindi Everton walipoichapa Southampton Bao 2-1.
Hilo lilikuwa Bao la Kwanza kwa Lukaku katika Mechi 6.
Everton walitangulia kupata Bao Mfungaji akiwa Fulbeki Seamus Coleman na Southampton kusawazisha kwa Bao la Gaston Ramirez alietokea Benchi.
Lakini Dakika 3 baada ya Southampton kusawazisha, Lukaku akafunga Bao la Pili na kuifanya Everton ikamate Nafasi ya 4 ingawa wanaweza kushushwa baadae leo ikiwa Liverpool watatoka Sare au kuifunga Chelsea huko Stamford Bridge.
VIKOSI: Everton: Robles, Coleman, Alcaraz, Distin, Baines, McCarthy, Osman, Naismith, Barkley, Oviedo, Lukaku
Akiba: Hibbert, Heitinga, Jelavic, Mirallas, Pienaar, Stones, Springthorpe.
Southampton: Kelvin Davis, Chambers, Fonte, Lovren, Shaw, Ward-Prowse, Cork, Rodriguez, Steven Davis, Lallana, Lambert
Akiba: Clyne, Yoshida, Ramirez, Gazzaniga, Hooiveld, Reed, Gallagher.
Refa: Mark Clattenburg
RATIBA MECHI ZIJAZO:
[Saa za Bongo] Jumatano Januari 1
1545 Swansea v Man City
1800 Arsenal v Cardiff
1800 Crystal Palace v Norwich
1800 Fulham v West Ham
1800 Liverpool v Hull
1800 Southampton v Chelsea
1800 Stoke v Everton
1800 Sunderland v Aston Villa
1800 West Brom v Newcastle
2030 Man United v Tottenham
MSIMAMO: HADI SASA MECHI YA LIVERPOOL NA CHELSEA IKIWA 0 - 0
NA | TIMU | P | GD | PTS |
1 | Arsenal | 19 | 19 | 42 |
2 | Man City | 19 | 33 | 41 |
3 | Liverpool | 19 | 23 | 39 |
4 | Chelsea | 19 | 14 | 37 |
5 | Everton | 19 | 13 | 37 |
6 | Man United | 19 | 10 | 34 |
7 | Newcastle | 19 | 5 | 33 |
8 | Tottenham | 19 | -5 | 32 |
9 | Southampton | 19 | 6 | 27 |
10 | Hull | 19 | -1 | 23 |
11 | Stoke City | 19 | -8 | 22 |
12 | Swansea City | 19 | -1 | 21 |
13 | Aston Villa | 19 | -7 | 20 |
14 | Norwich | 19 | -16 | 19 |
15 | West Brom | 19 | -5 | 18 |
16 | Cardiff | 10 | -15 | 18 |
17 | Crystal Palace | 19 | -16 | 16 |
18 | Fulham | 19 | -22 | 16 |
19 | West Ham | 19 | -10 | 15 |
20 | Sunderland | 19 | -17 | 14 |
CREDIT TO SOKA INA BONGO
Post a Comment Blogger Facebook
Toa Maoni Yako Kuhusu habari Hii
Note: Only a member of this blog may post a comment.