SNURA, AUNT EZEKIEL NA JACK WOLPER WAKATA MAUNO YA KUFA MTU HADHARANI

Mastaa wa filamu za Kibongo wenye jina kubwa mjini, Aunt Ezekiel, Jacgueline Wolper na Snura Mushi hivi karibuni walitisha kwa kufunga mtaa kutokana na mauno waliyokuwa wakikata mbele za wapiga ngoma wa Kundi la Baikoko, tukio lililojiri Mwananyamala, Dar nyumbani kwa msanii mwenzao Vanitha Omary.clip_image002Snura Mushi.

Wasanii hao waliwashangaza watu jinsi walivyokuwa wakijituma kukata mauno huku Wolper akimtunza mpiga ngoma na kumkatikia kwa staili mbalimbali zikiwemo za chumbani.

Aunt Ezekiel.

“Yaani wewe ulikosa mambo,  Snura alitoa shoo na mapacha wake utadhani alikuwa amelipwa, yaani walinogesha ngoma ya kumuaga mdogo wake Vanitha ambaye anakwenda kufunga ndoa Dodoma,” alisema sosi aliyekuwa akimsimulia mwandishi wetu.

Jack Wolper.

Aidha, wageni waliokuwa wamealikwa eneo hilo hawakudhani kama Wolper na Aunt wangeweza kujituma vile kama walivyokuwa wakikata mauno hayo kwa sababu ustaa wote waliuweka pembeni na kujiachia kwa raha zao.

SOURCE: BONGOCLANTZ.COM

Post a Comment

Hii ni Blog kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Nchi yetu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...

Previous Post Next Post