Unknown Unknown Author
Title: SHUKRANI: JOYCE KIRIA NA TIMU NZIMA YA WANAWAKE LIVE INATOA SHUKRANI ZA DHATI KWA WOTE WANAOTOA SUPPORT WANAWAKE LIVE
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Na Joyce Kiria Kipindio cha televisheni cha Wanawake Live kinapenda kuchukua nafasi hii kuwashukuru wadau wote kupitia mitandao yao katika ...

clip_image001Na Joyce Kiria
Kipindio cha televisheni cha Wanawake Live kinapenda kuchukua nafasi hii kuwashukuru wadau wote kupitia mitandao yao katika kutoa support na kutuunga mkono ili elimu tunayotoa ifike sehemu kubwa. Ni wadau wengi sana ambao wanashare kazi zetu hapa katika mitandao yao kama vile blogs, website, instagram, twitter, jamiiforums na hata habari nyingine kutumika katika magazeti, na hii itasaidia elimu kufika kwa watu wengi zaidi ambalo ndiyo lengo letu kubwa.

Hawa ni baadhi tu ya wadau wetu wanaotuunga mkono kwenye kurasa zao, www.jestina-george.com hii ni website inayomilikiwa na dada Jestina, kiukweli support yake ni kubwa mno mbali na kutumia website yake pia katika akaunti yake ya instagram anaweka vipindi vyetu. Mdau wa pili ni Global Publishers, hawa nao tunathamini support yao kama tunavyojua hapa nchini kwetu wapo watu ambao hawana access ya TV ila wana uwezo wa kusoma magazeti, Global wakiwa na magazeti pendwa kabisa yanayosomwa sehemu kubwa katika nchi yetu nao wanasaidia elimu hii kupatikana sehemu kubwa katika nchi yetu.

Wengine nimeweza kupata site zao kama www.iamallanlucky.webs.com Allan nae ni mdau wetu mkubwa, www.haki-hakingowi.blogspot.com, www.dirayadunia.blogspot.com, www.johnbadi.blogspot.com, www.lindiyetu.blogspot.com, www.sophiembeyu.blogspot.com, www.unapitwa.com, www.usipitwe.com, www.en-afrique.info, www.williammalecela.blogspot.com, www.eddymoblaze.blogspot.com, www.habarizetuleo.blogspot.com, www.dewjiblog.com, www.thechoicetz.com, www.bongoclantz.com, www.michuzijr.blogspot.com, www.issamichuzi.blogspot.com

Najua wapo wengine nao wana support ila inawezekana sikuzipata hizo site zao... Wakati tunaendelea kutoa shukrani kama nikizipata nitaziweka. Ila inawezekana pia ukanitumia.

Ila shukrani za dhati kabisa kwa wote wote wanaotuunga mkono katika harakati hizi za kuelimisha jamii kuhusu mchango mkubwa wa Wanawake katika jamii na kwa sababu hiyo tuna kila sababu ya kutokomeza  vitendo vyote vya ukatili wa kijinsia, kuhakikisha Mwanamke na mtoto wa kike anapata haki zake pamoja na kupata maendeleo kwa ujumla.

Nawapenda wote.

About Author

Advertisement

Post a Comment Blogger

Toa Maoni Yako Kuhusu habari Hii

Note: Only a member of this blog may post a comment.

 
Top