MHOLANZI Robin van Persie amezamisha klabu yake ya zamani, Arsenal akiifungia bao pekee la ushindi Manchester United na kuirejeshea matumaini ya kutetea ubingwa wa Ligi Kuu England.
Van Persie alifunga bao tamu kwa kichwa akiunganisha kona iliyochongwa kitaalamu na Wayne Rooney dakika ya 27 Uwanja wa Old Trafford. Sasa Timu ya Manchester united imepaa hadi nafasi ya tano katika msimamo wa ligi huku ikipitwa na arsenal wanao ongoza ligi kwa point 5 na chelsea kwa point 1.
matumaini ya kutetea yarejea kwa Manchester united kufuatia ushindi wa leo dhidi ya arsenal walio na kikosi bora kwa sasa kuliko manchester united walioonekana kupoteza dira katika mechi za mwanzo wa msimu huu na kocha David Moyes
Arsen Wenger akionesha nyuso ya huzuni katika mechi dhidi ya Manchester united leo timu yake ikiwa nyuma kwa bao moja lililofungwa na Mchezaji wake wa zamani Robin van Persie aliekuwa akizomewa na mashabiki wa timu hiyo katika kipindi cha kwanza cha mchezo huo, naye aliwajibu kwa kupachika bao maridadi mara baada ya kupokea kona nzuri iliyopigwa na Wyne Rooney naye kugonga kichwa na kutinga wavuni.
Kikosi cha United kilikuwa; De Gea, Smalling, Vidic/Cleverley dk45, Evans, Evra, Valencia, Jones, Carrick, Kagawa/Giggs dk78, Rooney na Van Persie/Fellaini dk85.
Arsenal; Szczesny, Sagna, Koscielny, Vermaelen, Gibbs, Arteta/Gnabry dk82, Flamini/Wilshere dk61, Ramsey, Ozil, Cazorla/Bendtner dk78 na Giroud.