“NIKOTAYARI KWENDA JELA KWA MTU ATAKAYE MDHALILISHA MAMA YANGU”–DIAMOND PLATNUM

DIAMOND 2STAA wa Bongo Fleva,Naseeb Abdul’Diamond amefunguka kuwa yuko tayari kwenda jela kama atatokea mtu yoyote akamchezea au kumdhalilisha kwa namna yoyote mama yake mzazi Bi.Sanura Kassim.

Akizungumza kupitia kipindi cha Take One cha Clauds TV na Zamaradi Mketema hivi karibuni alisema kuwa ni bora hao watu wakamchezea yeye(Diamond) hasa waandishi wanavyomdhalilisha kwenye magazeti kwa kuandika habari za uongo juu yake kuliko kumuandika na kumdhalilisha mama yake kwa habari za uongo.

‘Niko radhi kwenda jela kama itatokea kwa mtu yoyote yule akimdhalilisha mama yangu kwani nitamfanya kitu kibaya ambacho kitanifanya nishtakiwe na nipelekwe jela ni bora unichezee mimi kuliko mama yangu ni kila kitu kwangu sipendi mama yangu apate shida,alisema Diamond.

Pia alipoulizwa katika maisha yake aliwahi kwenda kwa mganga alisema kuwa hajawahi na kwamba haamini ushirikina na anamwamini Mwenyezi Mungu.

Post a Comment

Hii ni Blog kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Nchi yetu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...

Previous Post Next Post