Mkuu wa wilaya Ndg Kasimu Majaliwa alipotembelea Hospitali hiyo hivi karibuni, (picha na Maktaba)
Hospitali ya wilaya Ruangwa mkoani Lindi kwa muda mrefu
ilikuwa inakikabiliwa na tatizo la uhaba wa gari pamoja na shuka za
wagonjwa sasa limemalizika baada ya kupatikana kwa magari na shuka zaidi ya100 katika hospitali hiyo.
Gari na shuka hizo zenye thamani zaidi ya shs milioni 90 lilikabidhiwa kwa viongozi wa wilaya Ruangwa na mbuge jimbo hilo Kasimu Majaliwa katika hafla fupi iliyofanyika katika hospitali ya wilaya hiyo.
Kabla ya kukabidhi gari na shuka hazo mgeni rasmi ambaye ni mbunge wa jimbo hilo Kasimu Mjaliwa aliwataka watendaji kuhakikisha
kuwa wanatumia vifaa hivyo kwa malengo yaliyokusudiwa na sio kwa
matumizi mengineyo.
Majaliwa alisema kuwa gari hilo litapunguza matatizo ya usafiri kwa wagonjwa wa kutoka vijijini ambao kwa kipindi kirefu walikuwa wanasafirisha wagonjwa kwa kutumia baskeli na pikipiki.
Alisema kuwa serikali kwa kushirikiana na jamii itaendelea kutatua
kero na matatizo yanayowakabili wananchi kwa awamu ili kuhakikisha yana kwisha na kuwaletea maendeleo yao.
Majaliwa aliwata wananchi kutoa ushirikiano na viongozi na watendaji
kwa kuchangia miradi ya maendeleo ili kufanikisha mipango na
mikakati ya maendeleo iliyopangwa katika maeneo yao.
Post a Comment Blogger Facebook
Toa Maoni Yako Kuhusu habari Hii
Note: Only a member of this blog may post a comment.