Bw. Ally Mohamed Mtopa akifungua kikao cha Baraza la madiwani Halmashauri ya Kilwa hivi leo
Madiwani wakiwa katika Kikao cha Baraza la Madiwani Halmashauri ya Kilwa kikao kilichofunguliwa leo hii asubuhi
Na Abdulaziz Video.Kilwa
Baraza la Madiwani Halmashauri ya wilaya ya Kilwa kimekutana leo
katika kikao cha kawaida chini ya Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo,Bw Ally Mohamed Mtopa ambapo Madiwani wa Halmashauri hiyo wamemtaka Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo Bw Addoh Mapunda kutoa majibu ya Magari ya Halmashauri hiyo yaliyo katika karakana mbalimbali ili wajue hatma ya magari hayo ambayo yapo kwa muda mrefu huku shughuli za Halmashauri zikiendelea kukwama
Kufuatia hoja hiyo,Mkurugenzi aliwaeleza madiwani hao kuwa Kamati ya Fedha na Uchumi ilipitia kukagua magari hayo na kutoa Ushauri kwa Halmashauri hiyo kuuza magari hayo kutokana na uchakavu ili yanunuliwe magari mapya.