Baadhi ya Wafanyabiasha wakiwa mahakamani kujua hatma ya Mfanya Biashara Haji Mohamed Mpemba alieitwa mahakamani kujibu shitaka la kutolipa kodi ya Huduma ambayo wafanyabiasha wanaikataa kwa kutozwa nje ya Taratibu zilizopo.
Hii ndio hati ya wito wa mahakama kama inavyoonekana hapo juu ikimtaka Ndg Haji Mohamed mpemba kufika Mahakamani siku ya Jumanne Kwa madai tajwa hapo juu
Hatimaye Huduma imerejea kwa wananchi majira ya saa sita mchana kwa wafanya biashara hawa kufungua maduka na soko kuu Lindi huku wakisubiri maazimio ya kikao kilichofanywa kati ya uongozi wa jumuiya ya wafanya biashara na RPC wa Lindi ya ufuatiliaji wa malalamiko ya wafanya biashara ya kutozwa kodi ya huduma na Ongezeko la Kodi na Mashine za TRA.Baada ya Kufungua Maduka wananchi waendelea kupata huduma kama kawaida baada ya kuisha kwa kikao cha dharula cha uongozi wa umaja wa wafanya biashara na RPC.
Moja ya Stationery Kubwa Mjini hapa Ikiwa imefungua milango tayari kuanza kutoa huduma kwa wananchi mara baada ya kupatikana muafaka