AFYA::: UNAJUA SARATANI YA KIZAZI HUSABABISHWA NA NINI....?? SOMA HAPA NIKUJUZE

clip_image003Kama mwanaume ana mpenzi zaidi ya mmoja (ambaye ana chembechembe za saratani) na hukutana naye bila kuvaa condom, baada ya hapo aende kukutana tena kimwili na mwanamke wake tena bila condom hapo huchukuwa zile virus kutoka kwa mwanamke wa nje kupeleka kwa mwanamke wake wa ndani..!!

Kwa mwanamke ambaye ameanza kufanya mapenzi katika umri mdogo ambao mara nyingi ni chini ya miaka kumi na nane (18), ama kwa mwanamke mwenye wapenzi wengi pia huwa katika risk ya kupata saratani ya kizazi.

Na umasikini pia husababisha saratani ya kizazi haswa pale wanawake wanaotumia miili yao kufanya biashara ili kupata pesa za kujikimu.

Wanawake wanaovuta sigara pia huwa na risk kubwa sana ya kupata saratani ya kizazi. mwanamke kutokula mboga za majani na matunda husababisha risk ya kupata saratani ya kizazi.

DALILI ZA SARATANI YA KIZAZI:

  • kutokwa na damu zaidi ya kawaida wakati wa hedhi na -kukaa kwa mda mrefu
  • kutokwa na damu baada ya kukutana kimwili
  • kutokwa na majimaji mara nyingi sehemu ya mwanamke na yenye kutoa harufu mbaya
  • na kuumwa sana tumbo chini ya kitovu.

CHA MUHIMU KUFANYA..
kama hatuwezi kuwa waaminifu tuhakikishe tunatumia condom na tuhakikishe kama wanawake tuwe na mpangilio wa kwenda hospital na kucheki afya zetu na zaidi ya hapo kama wazazi tuwe wazi kwa wototo zetu kuhusu hili gonjwa.

Post a Comment

Hii ni Blog kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Nchi yetu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...

Previous Post Next Post