Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa
akijibu baadhi ya kero zilizoainishwa na Watumishi wa Umma katika
mfululizo wa ziara ya mkuu wa wilaya ya Ruangwa kutoa elimu ya Big
results now katika viwanja vya shule ya Likangara Ruangwa
Na Abdulaziz Video,Lindi
Walimu wa wilaya ya Rungwa,mkoa wa Lindi wamelalamikia uhaba wa nyumba za kuishi kuwa ni kikwazo cha utoaji wa taaluma na kuwaongezea ugumu wa maisha hivyo wameitaka halmashauri ya wilaya hiyo iwajengee nyumba kwenye shule zao ili kuepuka kuishi mbali na vituo vyao vya kazi kunakowasababishia kutumia gharama kubwa za usafiri.
Baadhi ya Waalimu waliohudhuria Mkutano huo
Walimu hao walitoa lalamiko hilo hivi karibuni kwenye mkutano na
mkuu wa wilaya Agnes Hokororo kwenye viwanja vya shule ya msingi ya Likangala ambapo alikutana na watumishi wa Tarafa ya Ruangwa
kuelezea mpango wa matokeo makubwa sasa (BIG RESULT NOW) kwenye wilaya hiyo.
Monica Chacky mwalimu wa shule ya sekondari ya Ruangwa alisema kuwa ukosefu wa nyumba za walimu hasa kwenye shule za sekondari na maeneo mengi ya vijijini kutokuwa na nyumba mzuri za kuishi kwa kiasi kikubwa kina wafanya walimu hao kuishi mjini na kulazimika kusafiri kila siku asubuhi na kurejea jioni baada ya kazi hali inayo wagharimu.
“Tatizo hili linatufanya kutumia kiasi kikubwa cha fedha kugharimia usafiri hasa wa bodaboda hivyo halmashauri ikishindwa kujenga nyumba basi itupatie fedha za kugharimia usafiri tunaoutumia”alisema Chacky.
Kiongozi huyo wa wilaya aliongozana na mkurugenzi mtendajiwa
halmashauri ndugu, Ruben mfune, pamoja na wakuu wa idara akiwamo Afisa elimu ili kujibu baadhi ya changamoto zilizoulizwa na watumishi waliohudhuria mkutano huo.
Nae Isack Mshimo mwalimu wa shule ya msingi Nangulugai alieleza kuwa changamoto inayotia hofu katika utekelezaji wa mpango huo katika sekta ya elimu kuwa, ni ukosefu wa nyumba za walimu na vyumba vya madarasa jambo ambalo usababisha darasa moja kutumika kuwa madarasa mawili.
“Kwa sasa tunalazimika kutumia darasa moja kwa mawili kutokana na tatizo la vyumba vya madarasa na kwa nyumba ulazimika kuishi nyumba za uswailini ambazo hazina hata usalama”alisema Mshimo.
Akijibu hoja hiyo kwa niaba ya afisa elimu, Afisa Elimu maalum Nd.
George Eraela alieleza kuwa serikali ina mipango madhubuti katika
kutekeleza ujenzi kwa kushirikiana na wizara pamoja na ofisi ya
mkurugenzi kutatua tatizo la nyumba za walimu na madarasa, na hivyo kuwaomba walimu kuvuta subira kwani jambo lipo katika utekelezaji.
Aidha mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya Ruangwa, Reuben Mfune alieleza kuwa kikwazo kinachosababisha utekelezaji kuwa ni
rasilimali chache zilizopo na kuwa halmashauri hiyo inatambua
upungufu wa madarasa 157 na kusema kuwa Fedha tayari imetengwa
kiasi cha sh mil 238 kwa ajili ya kutekeleza ujenzi wa nyumba za
walimu na madarasa.