Kiwanda Cha simenti cha Lindi kitakavyokuwa baada ya kukamilika Disemba, 2014
Na Said Hauni,Lindi.
UONGOZI unaojenga kiwanda cha Simenti mkoani Lindi
(Meis Industries Co.Ltd) umeeleza kwamba umenunua mitambo yenye
thamani ya Dola 25 milioni,sawa na Sh,4.10 bilioni za kitanzania, itakayofungwa kiwandani hapo mara baada ya kukamilika kwa ujenzi wake.
Hayo yameelezwa na Project meneja wa kiwanda hicho, Valelian Magembe wakati akitoa taarifa kwa Balozi wa nchi ya Comoro, nchini Tanzania, Islam Salehe, aliyetembelea mkoani humu kuona na kukagua maendeleo ya ujenzi.
Akiwasilisha taarifa hiyo, alisema tayari mitambo hiyo iliyonunuliwa Shanghai nchini China, imeshapakiwa kwenye meli tayari kuwasili nchini mwezi wa Novemba na Disemba mwaka huu.
Magembe alisema mitambo hiyo, itawasili kwa awamu mbili tafauti, ambapo awamu ya kwanza itawasili bandari ya Mtwara, Novemba 10 na mingine itawasili Disemba mwaka huu.
Alisema kiwanda hicho kimechelewa kuanza kutokana na changamoto
mbalimbali, zikiwemo milima eneo la kujengwa kwa kiwanda hicho pamoja na hali ya udongo wake aina ya mfinyanzi kuwa na tabia ya kupasuka wakati wa kiangazi na raini kipindi cha masika.
Magembe amemuelezea Balozi huyo kwamba kutokana na changamoto hizo, wamelazimika kuanza kuchonga mlima na kubadilisha udongo kwa kuondoa tabaka hilo na kuleta kifusi kingine.
Alisema
Kwa sasa tayari wameshaanza kupokea sehemu ya vifaa vitakavyotumika katika ujenzi wa Kiwanda hicho, zikiwemo Nondo na Saruji kutoka nchi za Pakstani na Uturuki.
“Baadhi ya vifaa vitakavyotumika kwa ajili ya ujenzi wake, kama vile Nondo kutoka nchini Uturuki na Simenti kutoka Pakstani zimeshawasili na vipo eneo la Saiti vikiendelea kufanyiwa kazi”Alisema magembe.
Magembe amemuelezea Balozi huyo wa Comoro, nchini Tanzania kuwa kiwanda hicho kinachojengwa na wataalamu wa kichina, kikikamilika kinatayarajia kuzalisha tani 600 hadi 700 za simenti kwa siku, huku kwa mwaka ni tani 1,080 hadi 200,000.
Naye, Balozi huyo wa Comoro,nchini Tanzania Salehe amesifu jitihada zinazofanywa katika kukamilisha kazi ya ujenzi wa Kiwanda hicho, ambacho kinatarajia kukamilika Decemba/2014, kitaajili watu
wapatao 2,000 wakiwemo wataalamu na wasiokuwa na utaalamu.
Katika ziara yake hiyo ya siku moja, Balozi huyo alikuwa ameongoza na Price mtoto wa Mfalume wa nchi yao ya Comoro pamoja na
ujumbe kutoka nchi ya Arabia, ambao ni wadau wa maendeleo.